Friday, August 27, 2021

DC MOYO:WAKURUGENZI WATAKAOKAIDI MAAGIZO YA LISHE KUCHUKULIWA HATU KALI ZA KIDHAMU

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akizungumza kwenye kikao kazi na wanawake vinara wa lishe bora namna ya kutafuta njia ya kutatua tatizo la udumavu mkoani Iringa

Baadhi ya wanawake vinara wa lishe bora wakiwa makini kumsikiliza meneja wa shirika lisilo la kiserikali la Save the Chidren mkoani Iringa John Masenza wakati semina ya kukabiliana na udumavu  mkoani Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mkoa wa Iringa umeziagiza halmashauri zote kuhakikisha zinatenga na kutoa fedha kwa ajili ya kupambana na tatizo la udumavu ambalo limekuwa linaleta doa licha ya mkoa huo kuwa mmoja ya mikoa ambayo inaongoza kwa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula.

Akizungumza kwenye mkutano na wanawake vinara wa halmashauri tatu za mkoa huo,mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya utolewa wa fedha kutoka kwa wakuu wa Idara mbalimbali za Halmashauri na kukwamisha mpango wa serikali ya mkoa kukabiliana natatizo la udumavu.

Alisema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu kwa mkurugenzi yeyote yule atakayekaidi agizo la kutoa fedha hizo kwa ajili ya kupambana na udumavu katika ngazi zote za halmashauri kama ilivyopangwa.

Moyo alisema kuwa haiwekani Halmashauri zote zimefanikiwa kutenga asilimia kumi kwa ajili ya makundi maalum ambayo ni vijana,wanawake na walemavu na kusindwa kutenga bajeti kwa ajili ya mpango wa uelimishaji jamii kuhusu lishe bora jambo ambalo linasababisha mkoa wa Iringa kuwa kinara kwa tatizo la udumavu.

“Mimi kama mkuu wa wilaya na kwa niaba ya mkuu wa mkoa nwa Iringa Queen Sendiga hatuweze kuendelea kuona tatizo la udumavu likiendelea huku wakurugenzi wakeindelea kuzembea kutenga na kutoa bajeti kwa ajili ya elimu ya lishe bora” alisema Moyo

Aidha Moyo amewaasa  wanawake vinara ambao walishiriki mafunzo lishe bora kuhakikisha wanaitumia vilivyo elimu waliyoipata kuhusu maswala ya lishe na kuwa mstari wa mbele kuielimisha jamii juu ya malezi stahiki ya watoto ikiwemo swala uzingatiwaji wa lishe bora.

Alisema kuwa anaamini kuwa wanawake ni jeshi kubwa hivyo wakiungana katika mapambano dhidi ya udumavu itasaidia kwa kiasi kikubwa kupuza au kumaliza kabisa tatizo la udumuvu na kuundosha mkoa wa Iringa katika aibu ya kuwa kinara wa tatizo hilo.

Moyo aliwataka watendaji wa Halmashauri zote za mkoa huo kuhakiksha wanapoanda mpango kazi wowote wahakikishe wanaweka agenda ya lishe inayolenga kuushusha mkoa wa Iringa katika nafasi ya udumavu ambao mkoa upo kwa hivi sasa ukiwa na kiwango cha asilimia 37.

Akizungumza kwa niaba ya wakurugenzi wote wa halmashauri za mkoa wa Iringa,mkurungezi wa Halmashuri ya manispaa ya Iringa Limbe Limbe alisema kuwa ameyapokea maagizo hayo na atayafikisha kwa wakurugenzi wote ili kuhakikisha mkoa wa Iringa unaondokana na tatizo la udumavu ambao limekuwa likiutia doa mkoa.

Limbe alipoungeza mradi wa USAID lishe endelevu  unaotekelezwa kupitia shirika la Diloitte kwa kuwezesha mafunzokwa jamii wakiwemo wanawake vinara wa Halmashauri tatu za mkoa wa Iringa kukabiliana tatizo la udumavu akitaja kuwa mpango huo ni chachu ya kufikia malengo ya kutokeza tatizo hilo. 

Kwa upande wake meneja wa shirika lisilo la kiserikali la Save the Chidren mkoani Iringa John Masenza alisema kuwa lengo la walisha hiyo ni kutafuta njia mbadala ya kuhakikisha wanatafuta namna ya kufikisha elimu ya lishe kwa jamii kwa ujumla.

Alisema kuwa wanawake vinara wa lishe wanauwezo mkubwa wa kufikisha elimu ya lishe kwa jamii kwa kuwa wanawake ndio wamekuwa nguzo ya familia katika mpangilio wa chakula kwenye familia nyingi za kitanzania na afrika lkwa ujumla.

Masenza alisema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa na maradi wa lishe endelevu unaofadhiliwa na USAID kupitia shirika lisilo la kiserikali la Diloitte ambalo lengo lao kubwa ni kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Iringa wanakuwa na elimu ya lishe bora ili kuondokana naudumavu uliopo.

No comments:

Post a Comment