Waziri wa Kilimo Mhe Prof.
Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa
habari wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika bandari ya Dar es
salaam tarehe 20 Julai 2021 kukagua hali ya upakuaji wa mbolea.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof.
Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa
habari wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika bandari ya Dar es
salaam tarehe 20 Julai 2021 kukagua hali ya upakuaji wa mbolea.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof.
Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa
habari wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika bandari ya Dar es
salaam tarehe 20 Julai 2021 kukagua hali ya upakuaji wa mbolea.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akizungumza na waandishi wa habari wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika bandari ya Dar es salaam tarehe 20 Julai 2021 kukagua hali ya upakuaji wa mbolea.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es Salaam
Waziri wa Kilimo Mhe Prof.
Adolf Mkenda amewasili nchini akitokea nchini Morocco ambapo pamoja na mambo
mengine katika ziara yake hiyo aliitembelea kampuni ya uuzaji wa mbolea ya OCP
ili kuendelea na mkakati wa serikali katika kuhakikisha kuwa mbolea inapatikana
kwa wingi nchini.
Akiwa katika ziara ya kikazi
ya siku moja katika bandari ya Dar es salaam tarehe 20 Julai 2021 Waziri Mkenda
amesisitiza kuwa Serikali inaendelea na mkakati wa kuhakikisha inadhibiti
ongezeko la bei ya mbolea.
Amesema kuwa bei ya mbolea
kwenye soko la Dunia imepanda kwa kiasi kikubwa hivyo serikali inaendelea na
juhudi za kuhakikisha kuwa bei ya mbolea nchini inaendelea kuwa katika
ustahimilivu wa bei huku juhudi zikiendelea za kuhakikisha bei ya mbolea
inashuka bei.
Amesema kuwa uingizaji wa
mbolea umeongezeka kwa kiasi kikubwa hapa nchini. “Hivyo natoa rai kwa
wafanyabiashara wa mbolea nchini wanaohifadhi mbolea wakidhani bei itapanda, hilo
hapana itashuka hivyo ni bora kuiuza mbolea hiyo mapema” Amekaririwa Waziri
Mkenda
Waziri Mkenda amesema kuwa
serikali haina kodi kwenye mbolea ila sehemu pekee ya gharama ilikuwa ni
ucheleweshaji wa kushusha mbolea pamoja na bei ya soko la Dunia. “Sijasema kwamba
bei ya mbolea itashuka sana maana bei imepanda Duniani” Amekaririwa Waziri
Mkenda
Waziri Prof. Mkenda ameongeza
kuwa Wizara yake tayari imefanya mazungumzo na Uongozi wa Bandari ya Dar es
salaam ili kuhakikisha kuwa mbolea inapowasili bandarini inapewa kipaumbele ili
iweze kupakuliwa kwa haraka na kuwafikia wakulima kwa wakati, “Kwa hili naomba
niipongeze Bandari ya Dar es salaam mmeendelea kusimamia kwa ufasaha swala la
upakuaji wa mbolea kwenye meli zinazowasili” Amesema
Ameongeza
kuwa ili kuhakikisha changamoto za wafanyabiashara zinapatiwa ufumbuzi kwa
haraka tayari Serikali imeshatoa maelekezo ya Mamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA)
kuanza kutoa vibali vya kuuza mbolea ambayo imeshaingia nchini (Export
Permit) badala ya vibali hivyo kutolewa ofisi ya Waziri wa
Kilimo kama ilivyokuwa awali.
Ameongeza kuwa ili kuongeza ufanisi
zaidi wa utendaji vibali hivyo vitatolewa kwa njia ya mtandao (Online) badala
yake Ofisi ya Waziri wa Kilimo itakuwa na jukumu la kupewa taarifa ya
utekelezaji wa utoaji vibali uliofanywa na TFRA.
MWISHO
No comments:
Post a Comment