Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo (wa tatu kulia) akishuhudia zoezi la kukabidhi hati za kimila kwa wananchi wa vijiji vya Nyang’hanga, Iseni na Lumeji vilivyopo katika Kata ya Sukuma katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza lililofanywa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akizungumza na wananchi wakati wa hafla ya kukabidhi hati miliki za kimila kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Magu mkoani Mwanza Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo kame Tanzania (LDSF) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akizungumza na wananchi wakati wa hafla ya kukabidhi hati miliki za kimila kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Magu mkoani Mwanza Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo kame Tanzania (LDSF) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Wananchi wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya kukabidhi hati miliki za kimila katika Halmashauri ya Wilaya Magu mkoani Mwanza kupitia Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo kame Tanzania (LDSF).
Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi waliokabidhiwa hati za kimila kupitia Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo kame Tanzania (LDSF).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo amewataka wananchi kutumia ardhi kufanya kilimo endelevu chenye kulinda mazingira.
Jafo amesema hayo leo Julai 9, 2021 wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kimila 750 kwa wananchi wa vijiji vya Nyang’hanga, Iseni na Lumeji Kata ya Sukuma katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza.
Alisema kuwa hivi sasa dunia katika maeneo kadhaa inakabiliwa na mabadiliko ya tabianchi hali inayosababisha kuwepo kwa changamoto mbalimbali za kimazingira ikiwemo ukame na mafuriko.
Hivyo Ofisi ya Makamu wa Rais imekuja na Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo kame Tanzania (LDSF) ambapo wananchi wa vijiji hivyo wamekabidhiwa hati hizo zitakazowasaidia kuedneleza ardhi hiyo.
“Ndugu zangu leo mna bahati ya kukabidhiwa hati za kimila ambazo ni jambo la msingi sana kwenu kwani zitawasaidia katika kuepukana na migogoro ya ardhi, hivyo niwaombe mtumie ardhi hiyo kufanya kilimo endelevu bila kuathiri mazingira,” alisema.
Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ambaye alikabidhi hati hizo alimuagiza Kamishna wa Ardhi wa Mkoa wa Mwanza kuhakikisha anatoa vyeti kwa vijiji vyote 23 ndani ya mwezi mmoja.
Lukuvi aliswma jukumu la kupanga matumizi ya ardhi katika halmashauri hiyo bado haijateklezwa kikamilifu kwa kuwa kati ya vijiji 82 ni vitano ndio vimeandaliwa mipango ya matumizi ambavyo ni sawa na asilimia 6.
“Kuna kazi kubwa kufanya kuhakikisha mnaandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ili kuwa na tija na pia kuepusha migogoro na jukumu la halmashauri ni kuandaa mipango hii,” alisema Waziri Lukuvi.
Aidha, alitahadharisha kuwa hati za ardhi kimila walizokabidhiwa hazitozwai kodi ya ardhji na wala hazina ukomo wa umiliki hivyo kuwataka walinde ardhi hiyo kufanya uzalisha hasa kilimo.
“Ndugu zangu mnahifadhi mazingira kwa ardhi yenu lakni niwasihi msiuze tumeiwekea sheria namba 5 ya mwaka 1999 hivyo mtumie kwa busara leo hii una ardhi kesho una watoto kumi utawarithisha nini,” alisema.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ardhi mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Iseni, Bw. Juma Kalumbete aliishukuru Serikali kwa kuleta mpango wa matumizi bora ya ardhi kupitia Mradi wa LDSF.
Alisema mpango huo unawasaidia kutumia ardhi vizuri kwa kilimo chenye tija tifauti nauleta mpango wa matumnizi bora ya ardhi ambapo hivi sasa watazingatia utunzaji wa mazingira.
“Naishukuru sana Serikali kwa kutukabdishi hati hizi za kimila kwani hapo zamani tulikuwa tunakata miti ovyo na kuchoma mkaa kwa hiyo sasa hivi tutaacha kukata miti ovyo,” alisema.
Bw. Kalumbete aliendelea kusema kuwa kwa kupitia hati hizo walizokabidhiwa wataweza kuchukua mikopo kutoka katika taasisi za kifedha na hivyo kuboresha maisha yao.
Mbali ya Magu Mradi wa LDSF unatekelezwa katika halmashauri za wilaya zingine za Mkalama (SINGIDA), Nzega (Tabora), Micheweni (Zanzibar) na Kondoa (Dodoma).
No comments:
Post a Comment