Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani,akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TANESCO wilaya ya Kongwa Shaban Seif wakati akikagua eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani Kongwa wakati wa ziara ya Waziri huyo iliyofanyika leo Julai 27,2021.
Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani,akizungumza na wananchi wa Mbande wakati wa ziara ya kukagua eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani Kongwa ziara iliyofanyika leo Julai 27,2021.
Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani,akimsikiliza Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Spika wa Bunge,Job Ndugai wakati akizungumza na wakazi wa Mbande wakati wa ziara ya kukagua eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani Kongwa ziara iliyofanyika leo Julai 27,2021.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani, ya kukagua eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani Kongwa ziara iliyofanyika leo Julai 27,2021.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mbande Bw.Peter Chiumbe akitoa kero ya umeme kwa Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani,wakati wa ziara ya kukagua eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani Kongwa ziara iliyofanyika leo Julai 27,2021.
Meneja wa TANESCO wilaya ya Kongwa Shaban Seif,akielezea hatua za ujenzi wa Kituo cha Kupooza umeme kilichopo Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa.
Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa mara baada ya kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O kinachotarajiwa kujengwa katika eneo hilo.
Na Zuena Msuya, Dodoma
Waziri wa Nishat,
Dkt.Medard Kalemani amesema Serikali itajenga kituo kikubwa cha kupoza Umeme
katika Wilaya ya Kongwa ili kumaliza tatizo la kukatika umeme mara kwa mara na
kuboresha upatikanaji wa Umeme katika wilaya hiyo na maeneo jirani.
Dkt. Kalemani
alisema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miundombinu ya umeme
ikiwa ni pamoja na kutembelea eneo litakalojengwa kituo hicho lililopo katika
Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni Wilayani ya Kongwa mkoani Dodoma,Julai
27,2021.
Katika ziara
hiyo, Dkt. Kalemani alisema kuwa tayari eneo la ukubwa wa Hekari 130
limepatikani ambalo litatumika kujenga kituo hicho, kitakachokuwa na uwezo wa
kufua umeme wa Kilovolti 220.
Aidha alisema
kuwa tayari zaidi ya shilingi milioni 63 zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa fidia
wakazi wa eneo hilo watakaopisha Ujenzi wa Mradi husika ambao utagharimu kiasi
cha shilingi Bilioni 41.2.
Ujenzi wa kituo
hicho unatajia kuanza kutekelezwa mapema mwezi Septemba mwaka huu 2021.
“Tuna umeme
mwingi sana Mkoa wa Dodoma, lakini kuna changamoto kubwa kukatika umeme na
wenye nguvu ndogo katika maeneo yote ya Wilaya ya Kongwa, kwa kipindi cha miaka
mingi sana, hii inatokana na umeme huo kusafiri umbali mrefu kutoka kituo cha
Zuzu hadi kufika huku takribani kilomita 120 na mzunguko ni takribani Kilomita
2000, suluhisho la kudumu ni ujenzi wa kituo cha kufua umeme ambacho kitamaliza
kabisa tatizo hilo na kuwa historia, hasa katika Viwanda, Wafanyabiasha na
watumiaji wengine”, alisema Dkt. Kalemani.
Hata hivo alisema
kuwa, katika kutatua tatizo la kukatika Umeme mara kwa mara katika maeneo ya
Mbande, Kibaigwa, Kongwa, Mpwapwa na Kiteto, ndani ya wiki hii kitafungwa kifaa
maalum, kinachojulikana kama AVR ili kuuongeza nguvu ya Umeme katika maeneo
hayo.
Dkt. Kalemani
alifafanua kuwa kifaa hicho tayari kimeshatoka mkoani Ruvuma kuja Dodoma na
kufungwa katika eneo la Mbande.
Sambamba na hilo
kazi ya Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme wa kV 220 inaendelea kujengwa
kutoka Zuzu kupitia Mpunguzi hadi kufika wilayani humo ili kupunguza tatizo la
kukatika kwa Umeme mara kwa mara katika maeneo tajwa na mengine jirani.
Ujenzi wa njia
hiyo ya umeme umefikia zaidi ya 55%.
Kufuatia
utekelezaji wa miradi hiyo, aliwataka wakazi wa maeneo hayo kuvuta subira
wakati tatizo la kukatika Umeme na kusambaza Umeme katika maeneo ambayo
hayakufikiwa likitatuliwa hivi karibu.
Aidha aliweka
wazi kuwa kuanzia mwaka wa fedha ujao, mkoa wa Dodoma utagawanywa Kitanesco na
kuwa kama majiji mengine ikiwemo Dar es Salaam kwa lengo la kuimarisha na
kuboresha huduma za umeme kwa wateja.
Vilevile alitumia
ziara hiyo kukipandisha hadhi kituo cha umeme cha Kibaigwa kuwa kituo cha
Wilaya ili kuimarisha na kuboresha upatikanaji wa umeme katika maeneo hayo.
Akizungumzia
suala la usambazaji wa umeme vijijini, Dkt. Kalemani alimtaka mkandarasi
kuongeza kasi katika kutekeleza kazi hiyo na kwamba wananchi wote waliolipia
waunganishiwe umeme kwa wakati.
Kwa upande wake,
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka aliwataka wakazi wa eneo litakalolegwa
kutuo cha kupoza umeme kuwa walinzi wa kituo hicho na kutoa ushirikiano kwa
watakaotekeleza kazi hiyo.
Vilevile
aliwataka wakazi wa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na umeme kujiandaa kuupokea
umeme huo kwa kutandaza nyaya katika nyumba zao pamoja na kulipia ili kuwa
tayari kuunganishiwa umeme.
Mkoa wa Dodoma
unawakandarasi 3 ambao watakaotekeleza mradi wa kusambaza umeme katika vijiji
vyote vilivyosalia kwa kipindi cha miezi 12 na kwa gharama ya shilingi 27,000
tu.
Mkoa wa Dodoma kwa sasa unaongoza kwa kuwa na megawati zaidi ya 640 za umeme ukifatiwa na mkoa wa Dar es Salaam wenye megawati zaidi ya 500.
No comments:
Post a Comment