Na Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU wa wilaya ya Iringa
amewataka watumishi na watendaji wote wa wilaya hiyo kuacha kufanya kazi kwa
mazoea katika kuwatumikia wananchi ambao ndio wameiweka madarakani serikali ya
awamu ya sita.
Akizungumza wakati alipomaliza
ziara ya kukagua miradi ya kimaendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa,mkuu wa wilaya Mohamed Hassan
Moyo alisema kuwa katika ziara ya kukagua miradi amegundua kuwa watumishi wengi wanafanya kazi kwa mazoea
katika vitengo walivyopangiwa.
Alisema kuwa watumishi wengi
bado hawazingatii muda wa kwenda kuwatumikia wananchi kwa kuwa wamekuwa
wanafanya kazi kwa muda ambao wanajitakiwa wenyewe tofauti na muda wa majukumu
wanayotakiwa kufanya kazi.
Moyo alisema katika miradi
mingi aliyoitembelea amegungua ucheleweshwaji wa kukamilika kwa miradi
kunatokana na watendaji wa serikali kutowasimamia vizuri wakandarasi ambao
wanakuwa wamepewa tenda ya kufanya kazi katika miradi husika a kimaendeleo.
Alisema kuwa wafanyakazi
walioajiriwa na serikali wanapaswa kufanya kazi kwa weledi unaotakiwa na kuacha
mara moja kufanya kazi kwa mazoea kama ilivyokuwa awali.
“Hiki ni kitabu kingine hivyo
umnatakiwa kufanya kazi kulingana na zama za kitabu husika ili kuendana na awamu
ya serikali ya awamu hiyo kwa lengo la kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ambao
ndio imechangia kuwepo kwa serikali ya awamu ya sita” alisema Moyo
Moyo alisema watumishi wote
wanatakiwa kufanya kazi kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha wanawatumikia
wananchi kama inavyotakiwa kulinga sheria za utumishi wa UMMA kwa lengo la
kuleta maendeleo kwa wananchi.
Alisema kuwa kwenye mikutano
yote watumishi nay eye mwenyewe wanatakiwa kufika kwa wakati na kuacha mara
moja tabia ya kuwakalisha muda mrefu wananchi wakiwasuburi viongozi kufika na
kuwapunguzia muda wa kufanya shughuli za kimaendeleo.
Kwa upende wao baadhi ya
watendaji wa mitaa,vijiji na kata pamoja na maafisa tarafa wa wilaya ya Iringa
wameahidi kuwa wataacha mara moja tabia ya kufanya kazi kwa mazoea ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya
sita kwa kuwatumikia wananchi.
Naye Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alisema kuwa atahakikisha anawasimamia watumishi wa Halmashauri hiyo ili waache tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi.
No comments:
Post a Comment