Thursday, July 29, 2021

DC MOYO: MWENGE WA UHURU KUTEMBELEA MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI SHILINGI BILIONI KUMI WILAYA YA IRINGA

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akimkabidhi mmoja ya wafanyakazi wa ofisini kwake Ramadhan Sosovele sare kwa ajili ya mapkezi ya Mwenge wa Uhuru ambao utakuwepo katika wilaya ya Iringa kwa siku Mbili kwa ajili ya kukagua,kuzingua na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi ya kimaendeleo.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MKUU wa wilaya ya Iringa amesema kuwa mwenge wa Uhuru unatarajia kutembelea,kuzindua,kuweka jiwe la msingi na kukagua jumla ya miradi kumi na nne ya kimaendeleo yenye thamani ya zaidi ya bilioni kumi kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya wilaya ya Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwa kwake mkuu wa wilaya hiyo Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuingia katika wilaya ya Iringa tareh 1/8/2020 ukitokea mkoa wa Dodoma kwa lengo la kukagua miradi ya kimaendeleo katika wilaya hiyo.

Alisema kuwa mwenge wa Uhuru unafaida kubwa kwa wananchi wa wilaya ya Iringa hivyo wananchi wanatakiwa kujitokeza kwenye maeneo ambayo mwenge wa Uhuru utakuwa unapita kwenye miradi au barabarani.

Alisema kuwa mwenge wa Uhuru utarajia kutembelea katika sekta zifutazo sekta ya kilimo,shamba la mboga mboga katika kijiji cha Kising’a,sekata ya miundombinu mwenge utaweka jiwe la msingi katika barabara inayopita Gangilonga hadi Kihesa,kukagua mfumo wa kufundishia wanafunzi wenye ulemavu,mradi wa maji Ismani Kilolo.

Moyo alisema kuwa ujio wa mwenge wa Uhuru ni fursa kwa wananchi wa wilaya ya Iringa kwa kufanya biashara mbalimbali kwenye maeneo ambaya mwenge huo utapita na kuwaongezea kukuza kipato cha wafanyabiashara hao.

“Wananchi wa wilaya ya Iringa changamkieni fursa ambazo zinakuja na mwenge wa Uhuru hasa kwenye biashara na elimu kwa kupeleka bidhaa katika maeneo ambayo mwenge utapita hata mjitokeze barabarani kuulaki mwenye wa Uhuru” alisema Moyo

Aidha katika ujio wa mwenge huo mkuu wa wilaya hiyo,Moyo amejitolea sare za mwenge bure kwa watumishi wote wa ofisi yake kwa lengo la kudumisha utumishi bora na kuongeza ushirikiano kazini kwa watumishi hao.

Alisema kuwa kuna watumishi ambao wanajitolea katika ofisi hiyo ambao hawawezi kununua sare hizo hivyo ameamua kujitolea kuwanunulia sare hizo ili watumishi wote waweze kuhudhuria shughuli za mwenge wa Uhuru utakapokuwa katika wilaya hiyo.

“Eee nimejitolea kwa kuwa mimi nauwezo wa kununua sasa kuna wafanyakazi hawana uwezo huo ndio maana nimeamua kujitolea kwa gharama zangu kuwanunulia sare hizo wafanyakazi wa ofisi hii ya wilaya kama ambavyo ofisi nyingine zimefanya”alisema Moyo

Kwa upande wao baadhi ya wafanyakazi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Iringa,walisema kuwa wanashukuru kwa sare hizo ambazo zitachangia kuongezeka kwa ushirikiano baina ya watumishi wa ofisi hiyo na mkuu wa wilaya hiyo.

Walisema jambo alilolifanya mkuu wa wilaya ni kuongeza hali ya kuwafanya wafanyakazi kuongeza bidii ya kufanya ya kwa kuwatumikia wananchi ambao ndio jukumu la namba moja kwenye utumishi wao serikalini.

No comments:

Post a Comment