Friday, July 23, 2021

CCM IRINGA WARIDHISHWA NA MIRADI INAYOTEKELEZWA MANISPAA YA IRINGA

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa,Abel Nyamahanga akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga wakati wa ziara ya kamati siasa ya chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa ya kukagua miradi ya kimaendeleo mkoani hapo
mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akinawa mikono kwenye moja ya maabara ya shule ya sekondari ya Mlamke iliyopo manispaa ya Iringa.


Na Fredy Mgunda,Iringa.

KAMATI siasa ya chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimeipongeza miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa kuwa na ubora unaotakiwa kutokana na dhamani ya pesa ambayo imetumika katika miradi hiyo.

Akizungumza wakati wa kukagua miradi ya maendeleo katika Manispaa hiyo Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa,Abel Nyamahanga alisema kuwa kamati imefanikiwa kutembelea  mradi wa uwanja wa ndege wa nduli,bweni la shule ya sekondari ya Nduli,barabara ya Gangilonga,Machinjio ya Ngelewala na maabara ya shule ya sekondari ya Mlamke wamekuta miradi hiyo imekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa.

Alisema kuwa kwa kipindi hiki ambacho manispaa ya Iringa inaongwa na madiwani wa chama cha mapinduzi imekuwa inatelekeza vilivyo miradi ya kukuza maendeleo kwa wananchi kwa kuitekeleza vilivyo Ilani ya chama hicho ya mwaka 2020 hadi 2025.

Nyamahanga alisema kuwa viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamefanya kazi kubwa kuhakikisha wanazitumia fedha za wananchi vizuri kwa kutekeleza ahadi za kutengeneza miradi kwenye ubora wake kulingana na dhamani ya fedha ambayo imetolewa kwenye mradi husika.

Aidha Nyamahanga alisema kuwa licha ya kuridhishwa na miradi mingi waliyoitembelea lakini wamekutana na miradi ambayo hawajaridhishwa nayo kutokana na kutekelezwa chini ya kiwango na mingine kuwa na mapungufu mengi ambayo wanatakiwa kulekebishwa haraka iwezekanavyo.

Alisema kamati haijaridhiwa na ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari ya Kleruu kwa kujengwa chini ya kiwango ukilinganishwa na thamani ya fedha ambayo imetumika kwenye maabara hiyo ukilinganisha maabara nyingine zilizojengwa kwenye shule nyingine.

Alisema kuwa katika mradi wa stand kuu ya mkoa wa Iringa kunachangamoto ambayo wananchi walitoa ardhi katika eneo la mradi bado hawajalipwa fidia zao ambazo wanadai hadi sasa wakati ofisi ya halmashauri ya Iringa ikiwa inazo pesa za kuwalipa wananchi hao.

Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Nduli, Ujenzi wa bweni la wanafunzi shule ya sekondari Nduli, Ujenzi wa Maabara shule ya sekondari Mlamke na Kleruu, Ujenzi wa barabara ya lami ya Kihesa, Kikundi cha vijana mafundi selemala ‘YOUNG FURNITURE GROUP’ cha Mlandege, Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kigungawe, Ujenzi wa jengo la abiria na utawala katika stendi mpya ya Igumbilo pamoja na Mradi wa Machinjio ya kisasa wa Ngelewala

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga alisema kuwa wameyapokea maagizo yote yaliyotolewa na kamati ya siasa ya chama chama mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa na watayafanyia kazi ili kuondoa kasoro ambazo zimejitokeza kwenye baadhi ya miradi ambayo kamati hiyo wameitembelea.

Aliwataka watendaji wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa weledi unaotakiwa ili kutumia fedha za wananchi vizuri kuendana na mradi ambao unakuwa unatekelezwa kwenye maeneo yao.

Naye Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alisema kuwa kamati ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari ya Kleruu na fundi aliyepewa kazi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaijenga upya maabara hiyo kwa kutumia fedha zao kwa sababu ya kujenga maabara hiyo chini ya kiwango huku serikali ikiwa imetoa fedha zote zinazohitajika.

Alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanatekeleza miradi yote kwa ubora na kubuni miradi mipya ambayo itasaidia kuchochea maendeleo ya wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndg. Omary Mkangama amesema moja ya sababu iliyopelekea kutokamilishwa kwa malipo ya fidia kwa wananchi waliojitolea maeneo ni kufungwa kwa mfumo wa malipo tarehe 30.06.2021 nchi nzima kwaajili ya zoezi la usuluhishi wa kibenki na maandalizi yakuingia kwenye mfumo mpya wa malipo MUSE ambapo zoezi hilo litakapokamilika ndio Halmashauri itaanza kulipa na wananchi watalipwa baada ya mfumo wa malipo kufunguliwa.

No comments:

Post a Comment