Meneja wa shirika lisilo la kiserikali la Save the Chidren mkoani Iringa John Masenza akiongea na washiriki wa mkutano wa wadau wa kutafuta njia za kupunguza udumavu mkoani Iringa.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa kutafuta njia za kupunguza udumavu mkoani Iringa.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa kutafuta njia za kupunguza udumavu mkoani Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
UNYWAJI wa pombe na kutokuwa na
elimu ya lishe kwa baadhi ya wananchi wa mkoa wa Iringa kumetajwa kusababisha
udumavu kwa watoto wadogo kutokana na wazazi wengi kutozingatia kuwapatia
vyakula vyenye lishe bora.
Akizungumza kwenye mkutano wa
wadau wa kutafuta njia ya kutatua tatizo la kuongezeka kwa udumavu,meneja wa shirika
lisilo la kiserikali la Save the Chidren mkoani Iringa John Masenza alisema
kuwa wananchi wa mkoa wa Iringa wanakunywa sana pombe na kusahau swala la
chakula kwa familia yake.
Alisema kuwa mkoa wa Iringa ni
mmoja ya mkoa ambao unazalisha chakula kwa wingi lakini tatizo kubwa limekuwa
kwa wananchi kuuza mazao hayo na kwenda kunywa pombe huku akisahau jukumu lake
la kuwapatia watoto chakula chenye lishe bora.
Masenza alisema kuwa wananchi
wanapokunywa pombe kwa wingi mara nyingi husahau kabisa swala la kwenda kula
kutokana na kuwa tayari anakuwa amelewa na hata kusahau kuwapikia chakula watoto
wadogo ambao aliwaacha nyumbani.
“Kumekuwa na tabia moja ya
wazazi kwenye vilabuni au kwenye bara na watoto wadogo na kuwanywesha pombe
jambo ambalo linapelekea watoto kupoteza hamu ya kula na kusababisha
udumavu kwa mtoto” alisema Masenza
Masenza alisema kuwa mradi wa USAID
lishe endelevu umejipanga kuhakikisha unachangia kupunguza udumavu kwa watoto
chini ya umri wa miaka mitano kwa lengo la kuboresha mifumo mbalimbali ya
lishe.
Alisema kuwa lengo la mradi wa USAID
lishe endelevu umejipanga kuhakikisha kuwa wanapunguza udumavu kwa asilimia
kumi na tano kwa kutoa elimu na kuboresha mifumo mbalimbali iliyopo katika
maeneo ambayo mradi unafanyika.
Kwa upande wake kaimu katibu
tawala wa mkoa wa Iringa,Elia Luvanda alisema kuwa mkoa wa Iringa unashika
nafasi ya tatu kitaifa kwa mikoa ambayo inaudumavu wa watoto wadogo kutokana na
wananchi wengi kutokuwa na elimu ya lishe.
Luvanda alisema kuwa hali ya
udumavu kwa watoto wadogo mkoani Iringa ipo kwenye asilimia 47 hali hii sio
nzuri kabisa kwa maendeleo ya kuwa na kizazi cha bora hapo baadae hivyo
wamejipanga kuhakikisha wanaboresha mifumo ya kiserikali ili kutoa elimu ya
lishe bora kwa wananchi wote.
Naye afisa lishe wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
Fanuel Nyandwike alisema kuwa wilaya hiyo inashida kubwa ya watoto wengi kuwa
na utapiamulo na kupelekea kuongezeka kwa udumavu kwa watoto waliopo katika
wilaya hiyo.
Alisema kuwa sababu kubwa ya kuongezeka
kwa udumavu inatokana na wazazi wengi kuwa walevi wa kupindukia na kusahau
majukumu ya kumulea mtoto kwa kumpatia chakula bora ambayo kina lishe ambacho
kitachochea kupuza udumavu kwa watoto.
Nyandwike alisema kuwa uongozi wa halmashuri ya wilaya ya kilolo umejipanga kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na sheria ndogo ya kuzibiti udumavu kwa kuwalazimisha wazazi kuzingatia kuwapatia watoto chakula chenye lishe bora.
No comments:
Post a Comment