Tuesday, June 8, 2021

SERIKALI KUANZISHA VITUO VYA KULEA VIPAJI KATIKA SHULE MBALIMBALI NCHINI-WAZIRI BASHUNGWA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Innocent Bashungwa akisisitiza jambo katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) inayofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.
Sehemu ya wanafunzi walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) inayofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Innocent Bashungwa katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) inayofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Innocent Bashungwa na Naibu Waziri wa TAMISEM katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) inayofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Innocent Bashungwa katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) inayofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.


Na Mwandishi Wetu, Mtwara

Serikali imeeleza kuwa inakusudia kuanzisha vituo vya kulea vipaji katika shule mbalimbali na katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya, Kilichopo Katika Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza ili kuhakikisha vipaji vya watoto havipotei.


Hayo yamesemwa Leo tarehe 8 Juni 2021 na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Innocent Bashungwa katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) na Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) inayofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.


Bashungwa amesema kuwa mashindano hayo ndiyo msingi wa kuvumbua vipaji na kwamba ili kufanya vizuri katika michezo mbalimbali, ni lazima uimara uanzie chini.


Aidha Waziri Bashungwa, amesema kuwa ili kukuza vipaji zaidi katika uzinduzi huo wamealikwa wavumbua vipaji kutoka vilabu mbalimbali nchini, Taasisi ya Mbwana Samatta na mawakala kutoka nchini Sweden.


Mashindano hayo yanaratibiwa na wizara tatu ambazo ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI). 


CHANZO: TBC ONLINE

No comments:

Post a Comment