Na Mwandishi Wetu, Rombo
Mbunge wa jimbo la Rombo ambaye ni Waziri wa
Kilimo Prof. Adolf Mkenda ametoa baiskeli 10 za walemavu katika jimbo lake la
Rombo kama sehemu ya ahadi zake za kusaidia makundi maalumu katika jamii.
Katika awamu ya kwanza, Prof. Mkenda alitoa
baiskeli 5 na awamu hii pia ametoa baiskeli 5 baada ya kuona kuwa bado kuna
uhitaji wa baiskeli hizo.
Baiskeli hizo zimekabidhiwa kwa wahitaji
kupitia kwa madiwani wa kata wanazotoka ili ziweze kuwafikia kwa urahisi.
Wakizungumza baada ya kupokea baiskeli hizo,
madiwani wa kata zilizopekea baiskeli hizo wamemshukuru Mbunge huyo kwa
kuendelea kuwakumbuka watu wenye mahitaji maalumu kwani wamekuwa katika kundi
lenye changamoto nyingi na hivyo kuhitaji msaada kutoka kwenye jamii ili
kukabiliana na changamoto hizo.
Mwananchi mmoja mwenye ulemavu wa viungo ndugu
Karoli Lyakurwa aliyefika na diwani wake kupokea baiskeli yake kutoka kwa
Mbunge amesema kuwa "Ninamshukuru sana Mbunge kwa kutukumbuka sisi
walemavu kwani tumekuwa tukisahaulika sana"
MWISHO
No comments:
Post a Comment