Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza katika Mkutano wa Uhamasishaji kwa Wadau kuhusu Mradi wa Gesi Asilia iliyosindikwa kuwa kimiminika (LNG), uliyofanyika Mkoani Lindi, Juni 20,2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio akizungumza katika Mkutano wa Uhamasishaji kwa Wadau kuhusu Mradi wa Gesi Asilia iliyosindikwa kuwa kimiminika (LNG), uliyofanyika Mkoani Lindi, Juni 20,2021
Picha za washiriki mbalimbali wa Mkutano wa Uhamasishaji kwa Wadau kuhusu Mradi wa Gesi Asilia iliyosindikwa kuwa kimiminika (LNG), uliyofanyika Mkoani Lindi, Juni 20,2021.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwa katika picha ya Pamoja na Wabunge wa kutoka Mkoa wa Lindi na Mtwara mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Uhamasishaji kwa Wadau kuhusu Mradi wa Gesi Asilia iliyosindikwa kuwa kimiminika (LNG), uliyofanyika Mkoani Lindi, Juni 20,2021.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwa katika picha ya Pamoja na viongozi wa Wizara na Taasisi zake mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Uhamasishaji kwa Wadau kuhusu Mradi wa Gesi Asilia iliyosindikwa kuwa kimiminika (LNG), uliyofanyika Mkoani Lindi, Juni 20,2021.
Hafsa Omar-Lindi
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema majadiliano ya utekelezaji wa Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) yatakamilika Oktoba mwaka na hatua ya ujenzi wa mradi huo utaanza mara moja.
Ameyasema hayo, Juni 20, 2021 wakati wa Mkutano wa Uhamasishaji kwa Wadau kuhusu Mradi wa Gesi Asilia iliyosindikwa kuwa kimiminika (LNG), uliyofanyika Mkoani Lindi.
Dkt. Kalemani amesema kuwa Timu ya maajadiliano baina ya Serikali na wawekezaji walipewa miezi sita kwaajili ya majadiliano ya utekelezaji wa mradi, na mpaka sasa imebaki miezi minne ili kukamilisha majadiliano hayo na kuanza rasmi kwa ujenzi wa mradi huo.
“Mhe. Rais amedhamiria mradi huu ujengwe kwa kasi na sisi tumejipanga kutekeleza maelekezo ya Rais lazima mradi wa LNG utekelezwe na utekezaji wake umeanza na majadiliano hayo ni hatua moja ya utekelezaji wake.” Alisisitiza Dkt.Kalemani.
Amesema kuwa, zaidi ya bilioni 56 zimetengwa kwaajili utekelezaji wa mradi na kuwataka wananchi wa Lindi na Mikoa ya jirani kutumia fursa mbalimbali ambazo zitapatikana kutokana na ujenzi huo.
Dkt.Kalemani amewatoa wasiwasi Watanzania wote na kueleza kuwa sababu zote ambazo zilisababisha mradi huo kuchelewa kwa utekelezaji wake kwasasa zimeshapatiwa ufumbuzi na hakutakuwa na sababu yoyote ambayo itachelewesha mradi huo.
“miradi hii mikubwa lazima iwe na manufaa kwa Serikali,wananchi na wawekezaji, kwahiyo tulikuwa tunapitia upya mfumo wetu wa uwekezaji ili makundi yote hayo yapate faida na hiyo ndio sababu ya kuchelewa lakini sasa tumeshaweka mfumo wetu sawa na ujenzi utaanza,”alisema.
Sambamba na hilo, Dkt. Kalemani pia amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC pamoja na wadau, kuanza mara moja utekelezaji wa uwekaji wa mipaka ya eneo ambalo litatumika kwaajili ya ujenzi.
Vilevile,amemtaka mkandarasi wa mradi wakati wa ujenzi kutumia vifaa vya ujenzi ambavyo vinazalishwa nchini ili kuinua masoko ya ndani.
Pia,amesema ujenzi wa mradi utasadia kuongezaka kwa pato la Taifa mara baada ya gesi hiyo kuanza kuuzwa nje ya nchi.
Katika hatua nyengine, amesema Serikali itaendelea kusambaza gesi majumbani na kwenye viwanda ili kuongeza wateja ambapo takribani viwanda 50 vinatumia rasilimali Gesi.
Dkt,Kalemani piaametoa wito kwa watumiaji wa Magari hasa Taasisi za Umma kununua magari yenye miundombini ya kuingiza gesi katika gari zao ili kupunguza gharama na kuboresha huduma zao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio amesema mradi utakuwa una faida nyingi kwa watanzania ambapo ameeleza kuwa Watanzania 15,000 watajiriwa katika hatua ya ujenzi na katika hatua ya uendeshaji Watanzania 5000 watajiariwa.
Pia, amesema faida ya nyengine itakayopatikana ni upatikanaji wa nishati ya uhakika kwaajili ya maendeleo ya viwanda na umeme na itasaidia kukuza uchumi wa nchi.
Nae,Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Shaibu Ndemanga ameipongeza Wizara ya Nishati kwa usimamizi mzuri wakati wa ukawagi wa fidia kwa wananchi wa Lindi na kuahidi kutoa ushirikiano katika kipindi chote cha ujenzi wa mradi huo.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Wabunge wa kutoka Mkoa wa Lindi na Mtwara,Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati, Adamu Zuberi,Kamishna Msaidizi wa Gesi Mhandisi Mohamed Fakihi na viongozi mbalimbali wa Wizara na Taasisi zake.
No comments:
Post a Comment