Friday, March 19, 2021

MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN AAPISHWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kilichotokea tarehe 17 Machi 2021 mkoani Dar es Salaam. Hafla ya Uapisho imefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akila Kiapo cha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo tarehe 19 Machi 2021 Ikulu jijini Dar es salaam.  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akielekea katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupewa Heshima ya kupigiwa Wimbo wa Taifa pamoja na kukagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati akipigiwa Wimbo wa Taifa mara baada ya kuapishwa kuwa Rais. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshma lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Mama Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
akiongea baada ya kuapa Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2021 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiongoza kuomba dua alipokwenda kumpa pole Mama Janeth Magufuli mara tu baada ya kuapa Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2021 Pamoja naye ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Bashiru Ally na Binti wa Marehemu Rais Dkt John Pombe Magufuli 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri leo tarehe 19 Machi 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa kuwa Rais. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment