Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 kwa mafungu sita (6) yaliyochini ya ofisi hiyo wakati wa kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichofanyika tarehe 28 Machi, 2021 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria Mhe. Mohamed Mchengerwa akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kamati hiyo wakati wa kikao cha kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 hii leo Bungeni Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu)Mhe. Ummy Ngeriananga akieleza mikakakti ya kuwezesha watu wenye ulemavu na kusimamia haki zao wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia kikao cha Kamati hiyo leo Machi 28, 2021.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Ng’wasi Kamani akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Khadija Shaban akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Watendaji pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo wakifuatilia kikao hicho.
Sehemu ya Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hoja wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipokutana hii leo Bungeni Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja za wajumbe walizohoji wakati wa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 wakati wa kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichofanyika tarehe 28 Machi, 2021 Jijini Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment