JUMUIYA ya Alfirdaus ya Jijini Dar es salaam imeendelea kutekeleza harakati zake za kusaidia jamii ikiwemo uchimbaji wa visima virefu vya maji katika maeneo mbalilmbali hapa Nchini
Akizungumza katika ufunguzi wa msikiti Alnoor Uliopo Msakangoto Sahare Jijini Tanga Afisa Mipango wa taasisi hiyo Zack Naseer Ruqeish amesema kuwa hivi sasa wamefanikiwa kuchimba visima zaidi ya elf saba katika maeneo mbalimbali hapa nchini
Zack Amesema kuwa lengo la jumuiya hiyo ni kuisaidia jamii ya kitanzania katika Nyanja mbalimbali za huduma ya Kijamii ambapo kwa hivi sasa wanaendelea na Ujenzi wa jengo la Waqfu la Ghorofa saba Jijini Dar es salaam ambalo litakuwa ni kitega uchumi cha kuisaidia jamii.
Kwa upande wake katibu Mkuu wa Taasisi ya Alfirdaus Saleh Alhinai amesema kuwa pia Taasisi hiyo hivi sasa inawahaudumia watoto yatima hivyo kuomba jamii ya kitaanzia kuzidi kuwaunga Mkono katika harakati hizo kwa kutoa michango yao ili kuwawezesha kuwafikia watu wengi zaidi
Akizungumza katika Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdulrahman Shiloow ameitaka jamii ya Kiislam kujitolea katika mambo ya kher ikiwemo kuwaanda watoto wao katika suala hilo la kutoa sadaka
Aidha viongozi wa Jumuiya hiyo ya Firdaus wamesema kuwa zaid ya shilingi milion mia mbili zimetumika katika ujenzi huo uliohusisha msikiti, chumba Cha kuoshea maiti pamoja na ukarabati wa madrasa katika eneo hilo la msakangoto.
Katika risala ya shukran kwa wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa msikiti huo utaondosha changamoto ya sehemu nzuri ya kufanyiwa ibada.
No comments:
Post a Comment