Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Karagwe na Diwani kata ya Nyaishozi, Mhe. Wallace Mashanda akisisitiza suala wanafunzi kupatiwa huduma ya uji na chakula mashuleni katika mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mhe. Innocent Bashungwa katika kata ya Nyakasimbi, jimboni Karagwe, Januari 03, 2020.
Ikiwa ni Mwendelezo wa ziara za Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mhe. Innocent Bashungwa katika vijiji vya kata zinazopatika jimboni Karagwe ambazo zimekuwa na lengo la ya kutoa shukrani kwa wananchi kwa ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi uliofanyika Octoba 28, 2020, Kusikiliza na kuweka mikakati ya kutatua changamoto mbalimbali lakini pia kukagua miradi ya maendeleo katika kata husika.
Wananchi katika kata tofauti wa jimbo la Karagwe wamejitokeza mbele Mhe. Bashungwa kulalamikia maafisa kutoka ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuwatakisha pesa (rushwa) ili kuwalahisishia zoezi la upatikanaji wa namba za vitambulisho vya Taifa pindi wakifika katika kata zao kwa ajiri ya kuwasaidia kwenye zoezi la kujiandikisha na kupatikana kwa vitambulisho vya Taifa.
Awali katika ziara hiyo, Mzee Byekwaso Kutoka kata ya Kanoni ameajitokeza mbele ya Mhe. Bashungwa kuwasilisha shida wanazozipata kwenye uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa huku akieleza kukithili kwa vitendo vya rushwa katika zoezi hilo
“Sisi huku tumechukua muda mwingi kwenda kusajili, tumemaliza siku tano pale Rwambaizi, wakati wanaleta namba za NIDA wengi hatukupatikana kwenye orodha, lakini pia tunatopokuwa kwenye usajili kuna watu wanataka uwape hela, kweli hiyo hela imetuletea nongwa, Kwahiyo Mheshimiwa Mbunge hayo mambo ya NIDA yanaonekana kama hewa tu, wanaopata namba ni wale wenyenacho sisi ambao hatuna hicho hatukupata hizo namba” amesema Mzee Byekwaso
Sambamba ya hayo, Pia katika kata ya Nyakasimbi Mama aliyetambulika kwa jina la Mama Edina amejitokeza mbele ya Bashungwa huku akiwasilisha kero yake ya kulalamikia zoezi la upatikanaji wa namba za Vitambulisho vya Taifa ambapo walijitokeza kujisajili lakini mpaka sasa hawajapata namba hizo hadi imepelekea kufungiwa kwa laini zao za simu kitu ambacho kimesababisha kukosa mawasiliano na ndugu zao.
Wakati akijibu maswali, Kero na Changamoto Mbalimbali Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mhe. Innocent Bashungwa katika Kata ya Ihembe Januari 03, 2021 imemulazimu kumpigia simu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) huku wananchi wakisikiliza na kuwasilisha kero ambazo amekuwa akizipata kutoka kwa wananchi katika mikutano ambayo amekuwa akifanya katika kata mbalimbali.
“Mkurugenzi nipo kwenye mkutano katika kata ya ihembe, jana nilikuwa na mkutano kata Igurwa na Kanoni lakini kila mkutano wananchi wanapongeza juhudi za Serikali kwenye kutatua changamoto lakini kwenye NIDA mmekuwa majipu, Cha kwanza wananchi wanalalamikia mwenye hela ndiye anayepata namba ya NIDA, cha pili hata ambao wamedhibitishwa bado wanazungushwa, Kwahiyo Mkurugenzi mimi nakuagiza kwa upande wa Karagwe fatilia maafisa wako hawatoshi hatuna Imani nao huku.” amesema Mhe. Bashungwa wakati akiongea na Mkurugenzi mkuu wa NIDA.
No comments:
Post a Comment