Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akiwahutubia Warajis Wasaidizi wa mikoa ya Tanzania Bara Januari 6, 2021 katika hafla ya kukabidhi vitendea kazi yakiwemo magari pamoja na kompyuta katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika Jijini Dodoma.
Waziri
wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akimkabidhi Mrajis Msaidizi wa mkoa wa Simiyu
Bwana Ibrahim Kadudu gari aina ya Nissan Hard N 300 Double Cabin 4WD Januari 6,2021 katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika Jijini Dodoma.
Waziri
wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na
Rais Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kurudisha heshina na hadhi ya Ushirika
na ndiyo maana hatua kadhaa zimeanza kuchukuliwa ikiwemo ya kurejesha mali za
Ushirika zilizoporwa zenye thamani ya zaidi ya Bilioni 61.
Waziri
wa Kilimo Prof. Mkenda ameyasema hayo Januari 6, 2021 wakati
akiwakabidhi Warajis Wasaidizi magali mapya manne yenye tahamani ya shilingi
milioni 275 katika Ofisi za Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Jijini Dodoma.
Waziri
Mkenda amesema kabla Tazania haijapata uhuru; Tasnia ya Ushirika ilikuwa
ikifanya vizuri na kutoa mfano wa Chama Kikuu cha Ushirika cha mkoa wa
Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperatives Union – KNCU) kilichokuwa kikiwaunganisha
Wakulima wa zao la kahawa na kuongeza kuwa kilianzishwa mwaka 1925 na kwamba
Barani Afrika Tanzania ilifanya vizuri kiasi cha nchi nyingine kuja kujifunza.
Waziri
Mkenda ameongeza licha ya KNCU kufanya vizuri Shirikisho la Vyama vya Ushirika
kutoka Kanda ya Ziwa (Victoria Federation) nayo ilikuwa mfano wa kuigwa katika
Bara la Afrika katika miaka ya hamsini (1950s) na kuongeza kuwa juhudi
zinazofanywa katika Awamu ya Tano lengo lake ni kurejesha heshima na hadhi hiyo
ili kuleta mapinduzi ya kweli kwenye Sekta za Kiuchumi Sekta ya Kilimo ikiwa ni
miongoni mwao.
Prof.
Mkenda ameongeza kuwa ili kurejesha hadhi hiyo; Wizara imeandaa mpango wa
kuipitia upya Sheria ya Vyama Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 ili kuifanyia
marekebisho iendane sawa na mahitaji ya sasa.
“Warajis
pamoja na Washiriki wa hafla hii; Wizara imeona ipo haja ya kuipitia upya
Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013. Mchakato wa kuipitia
utawashirikisha Wadau wote na hata wale magwiji ambao Ushirika ulifanya vizuri
wakati wao, tutakutana nao na watatupa maoni yao”.
“Kupitia
maoni ya Wadau ambayo yatakuwa shirikishi; Tutapata Sheria nzuri ambayo
itakidhi matakwa ya wakati na ambauo itajibu changamoto kadhaa tunazokutana
nazo kwa sasa”. Amekaririwa Prof. Mkenda.
Waziri
Mkenda amesema lengo la kufanya hivyo ili kuhakikisha Sheria mpya anajenga
mazingira wezeshi ya kuipeleka Tasnia ya Ushirika kwenye maendeleo ya kweli na
endelevu nchini.
Waziri
Mkenda ameongeza kuwa jambo lingine ambalo Serikali kupitia Wizara ya Kilimo
kama msimamizi wa Tasnia ya Ushirika ni kuendelea kupambana na Wezi na
Wabadhirifu wa mali za Wanaushirika.
“Tutaendeleo
kupambana ili kuondoa wizi na ubadhirifu; Ofisi ya Waziri Mkuu imetusaidia sana
kupambana na ubadhilifu. Nawaomba Warajis Wasaidizi tusaidiane kwenye jambo
hilo”.
Waziri
Mkenda ameongeza kuwa ili kuendelea kurejesha hadhi na heshima ya Ushirika
nchini Wizara itaendelea kuwajendea uwezo Wasimamizi katika Tasnia kwa kuwa huko
udhibiti na usimamizi ni jukumu la muhimu kwenye maendeleo ya tasnia ya
Ushirika.
“Ndugu
zangu kuna haja ya kufanya maboresho makubwa kwenye utunzaji wa kumbukumbu;
Kumbukumbu zisipokaa vizuri tutakuwa na changamoto kubwa kwenye usimamizi na
udhibiti kwa kuwa hayo ni moja ya majukumu ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika.”
Amekaririwa Waziri Mkenda.
Waziri
Mkenda ameongeza kuwa kwenye eneo la utunzanji wa kumbukumbu usioridhisha
umetia doa utendaji wa Vyama vingi vya Ushirika kwenye Taarifa ya Shirikisho Ukaguzi
la Vyama vya Ushirika nchini (COASCO).
Waziri
Mkenda ametolea mfano Vyama Vikuu vya Ushirika 43 havijapata hati safi na
ukiangalia siyo kwamba kuna wizi ila Wasimamizi hawakuwa na uwezo wa kuweka
kumbukumbu vizuri
Katika
taarifa ya COASCO jumla ya Vyama vya Akiba na Mikopo 3,374. Ni Vyama 34 tu
ndivyo vimepata hata safi ila ukiangalia siyo Vyama vyote vya Akiba na Mikopo
fedha za Wanachama vimeibwa ila ni uwekaji wa taarifa za hesabu na kubukumbu
hazijawekwa vizuri.
Wakati
huohuo Waziri Mkenda amevipongeza Vyama Vikuu vya Kahama (Kahama Cooperatives
Union – KACU) na Chama Kikuu cha Wilaya ya Karagwe na Missenyi (Karagwe
Cooperative Union – KDCU) kwa kufanya vizuri kwenye tasnia ya ushirika wa
mazao, hususan zao la kahawa.
“Vyama
hivi vimekuwa kielelez na sote tunapaswa kuwapongeza; Walichofanya vizuri
Karagwe na Kahama. Tunapaswa tukiige kote nchini. Vyama hivi vimetupa matumaini
makubwa.” Amekaririwa Waaziri Mkenda.
Aidha
Waziri Mkenda amepongeza Wanachama na Uongozi wa Chama cha Ushirika wa Wakulima
wa Kahawa wilaya ya Rombo (MAMSELA AMCOS) pamoja na Chama cha Ushirika wa
Mpunga Bonde la Mto Ruvu (CHAURU) kwa kufanya vizuri na kuwa mfano wa kuigwa.
Aidha
Waziri Mkenda amekipongeza Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Korosho wa
Wilaya ya Nanyumbu, Masasi na Mtwara Cooperative Union (Nanyumbu, Masasi and
Mtwara Cooperative Union - MAMCU).
“Chama Kikuu cha MAMCU kimefanya vizuri; tunatakiwa wote tujifunze kutoka kwao, wanauza mazao mapaka nje ya nchi, wanasimamia ubora za zao la korosho.” Amesisitiza Waziri Mkenda.
No comments:
Post a Comment