Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya amesema migogoro yote inayohusu leseni za uchimbaji madini lazima zitatuliwe kupitia Tume ya Madini ambayo ndio taasisi yenye dhamana ya utoaji leseni hapa nchini wakati alipokutana na Viongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa Mwime 2 katika Ukumbi wa Mikutano wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Jijini Dodoma.
Prof.
Shukrani Manya amewataka Viongozi wa
Mgodi wa Mwime 2 kufuata Sheria na Taratibu zilizowekwa na Wizara ya Madini
wakati wanapohitaji leseni kwenye maeneo
ya uchimbaji ili kuondoa migogoro inayojitokeza mara mara.
Ametoa
maelekezo hayo leo, Januari 25. 2021 wakati alipokutana na Viongozi wa Mgodi wa
Mwime 2 wakiongozwa na Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa mgodi huo kutoka Kahama Mkoani Shinyanga ambapo wamefika
ofisini kwake kupata maelekezo ya sababu ya ucheleweshwaji wa maombi ya leseni
ya Mgodi wa Mwime 2.
Naibu Waziri ametoa maelekezo hayo baada ya kuelezwa migogoro waliyonayo na Ofisi ya Madini wilaya ya Kahama kuhusu ucheleweshwaji wa kupatiwa namba ya malipo “control number” kwa ajili ya kupatiwa leseni halali ya eneo la machimbo yaliyopo Mwime 2.
“Historia
ya mgogoro wa Mwime 2 ni wa muda mrefu toka nikiwa kwenye nafasi ya Katibu
Mtendaji wa Tume ya Madini. Mimi ndiye niliyepitia leseni zenu tatu
mnzazozitumia sasa. Kwa hiyo historia
yenu yote ninaitambua. Ni vema mkafuata
Sheria na Taratibu zilizowekwa na Wizara kupitia watoa leseni Tume ya Madini.”
Aidha,
Naibu Waziri amewataka Viongozi hao wa mgodi wa Mwime 2 kusubiri kikao cha
kamati ya wilaya ya Ulinzi na Usalama kitakachoongozwa na Mkuu wa wilaya mapema
Mwezi Februari, 2021 kwa ajili ya kutoa maamuzi ya mgogoro huo. Pia amewaeleza
ili kuondoa migogoro hii mara kwa mara ni vyema kupokea maelekezo kutoka kwa afisa
madini mkazi na kuyafanyia kazi kabla ya kuamua kuonana na Waziri mwenye
dhamana kwanza.
Mhandisi
Yahaya Samamba akipokea maelekezo toka kwa Naibu Waziri amesema suala hilo
analifahamu. “Ni vyema tukasubiri maelekezo ya kamati ya Ulinzi ya wilaya na kwa
sababu nyinyi ndio watu wa mwanzo wa eneo hilo kuanza kufanya kazi nina imani
mtapewa kipaumbele kuliko kugawa eneo kwa watu wageni kutoka nje ya Shinyanga”.
Amesisitiza Sambamba
Naye,
Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi wa Mgodi wa Mwime 2, Emmanuel Mlimandago amesema
wanaiomba Tume ya Madini iwasaidie kutatua mgogoro huo ili wapate leseni ya
kuendelea kuchimba katika eneo hilo.
“Tumeboresha miundombinu ya barabara katika
maeneo yanayozunguka mgodi wa Mwime 2. Awali kulikuwa na changamoto ya mgodi
kuingiliwa na maji lakini tuliweka juhudi ya ujenzi wa tuta kubwa ambalo limekuwa msaada mkubwa
katika kazi zetu”. Amesema Mlimandago
Pia,
Afisa Mahusiano wa mgodi wa Mwime 2 Christopher Bundala amemuomba Prof. Manya
kumuelekeza Kaimu Mtendaji wa Tume ya Madini Yahaya Samamba kutembelea mgodi wa
Mwime 2 wilayani Kahama ili mgogoro huo uweze kutatuliwa vizuri. Amesema ni
vyema Tume ya Madini ikatutembelea ili isikilize pande zote za mgogoro huu
kabla ya kutoa maamuzi.
No comments:
Post a Comment