kocha wa timu ya Mtwivila city (Ifuenga )Edger Nzelu akiongea na wachezaji wa timu hiyo.
Kocha wa timu ya mtwivila city ( Ifuenga) ameahidi kuwa kesho timu ya mtwivila city itaifunga timu ya Irole katika michezo wao wa nusu fainali ya pili itakayofanyika katika uwanja wa Mkwawa na kuifuata timu ya Ivambinungu ambayo imetangulia tayari fainali ya ligi ya mkoa wa Iringa (Asas super league) 2020/2021.
Akizungumza kwa njia ya simu kocha wa timu ya Ifuenga Edger Nzelu alisema kuwa timu hiyo imejipanga vilivyo kuhakikisha wanashinda mchezo huo muhimu ambao kwa namna yoyote ile lazima washinde kwenda fainali.
Alisema baada ya mchezo wa kwanza kutoka bila kufungana katika uwanja wa nyumbani wa timu ya mtwivila city (Ifuenga) inatokana na aina ya uwanja ambao wanaoutumia hivyo kwenda kuutumia uwanja wa mkwawa utawapa fursa wachezaji wa timu hiyo kucheza mchezo waliozoea.
Nzelu aliongeza kuwa baada ya nusu fainali ya kwanza wachezaji wa timu hiyo wameahidi kujituma kuhakikisha wanashinda mchezo huo muhimu ili kufika fainali ya ligi ya Asas super league.
Naye mfadhili wa timu hiyo Joseph Kilienyi alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo wa kssho na kufika fainali na kuchukua kombe hilo.
Alisema kuwa timu ya Irole ni timu nzuri lakini wao wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo muhimu kwao kwa kuwa wanataka kwenda kanda na kuhakikisha timu hiyo inafika katika madaraja ya juu na hatimaye kufika ligi kuu Tanzania Nara.
Timu ya mtwivila city (Ifuenga) imejipanga kwa kila kitu hivyo wakiwa mabingwa wa mkoa watahakikisha timu hiyo hairudi nyuma tena kwenye ligi ya mkoa wa Iringa tena.
No comments:
Post a Comment