Sunday, January 10, 2021

DKT JINGU AITAKA JAMII YA KIMASAI KUTUMIA UTAMADUNI WAO KUWA FURSA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt John Jingu akisalimiana na wajasiriamali Wanawake wa kikundi cha Ereto kilichoko Minjingu Kata ya Nkait Wilayani Babati, Manyara. 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu ameitaka jamii ya kimasai nchini kutumia Utamaduni wao kama fursa ya kujiongezea kipato na  kujiimarisha kiuchumi. 

Dkt. Jingu ameyasema hayo alipotembelea Kikundi cha wajasriamali Wanawake cha Ereto kilichopo Kijiji cha Minjingu Kata ya Nkait Wilayani Babati Mkoani Manyara kuona shughuli wanazozifanya.

 

Dkt. Jingu amesema jamii ya kimasai imezungukwa na fursa nyingi ikiwemo Utamaduni wa Jamii hiyo ambao umekuwa ukijinadi ndani na nje ya mipaka ya nchi.

 

Hata hivyo, amesema jamii husika bado haijaitumia fursa hiyo ipasavyo kuutangaza na kuufanya kuwa chanzo cha kiuchumi.

 

" Watu wa mataifa mbalimbali duniani wanasafiri na kuja Tanzania kuja kuangalia tamaduni zetu na zimekuwa kivutio kikubwa sana kwao, tutumie fursa hii kutengeneza pesa" alisema

 

Ameongeza kuwa jamii hiyo inatakiwa kuboresha bidhaa wanazozitengeneza kitamaduni ili ziweze kupanua wigo na soko la Kimataifa.

 

" Katika hili naomba Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo nchini SIDO na wengine kusaidia vikundi hivi kuwa na bidhaa zilizo bora ili kuongeza soko lake" alisema 

 

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati John Nchimbi amemhakikishia Katibu Mkuu Dkt. Jingu kuwa Halmashauri hiyo itaendelea kusimamia mikopo mwa makundi husika kwa kutenga ya asilimia 10 ya mapato yake ili iweze kunufaisha wanufaisha walengwa.

 

Akisoma Taarifa ya Wilaya ya Babati, Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Stedvant Kileo amesema katika robo ya mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri hiyo imetoa jumla ya shilling Millioni 117 kwa vikundi vya Wanawake Wilayani humo.

 

Akiwasilisha mafaniko na changamoto ya Kikundi cha Wanawake wajasiriamali cha Ereto mmoja wa mjumbe wa Kikundi hicho Jesca Kipara ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwawezesha Wanawake muwawezesha kushirikiana wenza wao kulea familia.

 

" Mikopo hii imetusaidia sana katika masuala ya kifamilia kwani kwa tamaduni zetu kuna wakati wa kiangazi wanaume wanasafirisha mifugo kutafuta malisho kwa mifugo kwa hiyo pesa tunazopata zinasaidia kulea familia kipindi wanaume hawapo" alisema 

No comments:

Post a Comment