Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akipata maelezo juu ya Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kianga kutoka kwa Mkurugenzi wa Uratibu shughuli za Serikali – SMZ Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bw. Khalid Khalid Hamrani Mkurugenzi, hii leo Zanzibar. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Uwakilishi (Mwera) Mhe. Mihayo Juma N’hunga na wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mwera Mhe. Zahor Mohamed Haji.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu akipata maelezo juu ya Ujenzi wa
Bwalo la Mitihani kwa wafunzi (halipo pichani) kutoka kwa Mkurugenzi wa Uratibu shughuli za
Serikali – SMZ Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bw. Khalid Khalid Hamrani
Mkurugenzi, hii leo Fujoni Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu amesema watanzania wote wanao wajibu wa kujivunia matunda ya Muungano ikiwa ni pamoja na miradi ya Maendeleo inayotekekezwa pande zote mbili za Muungano.
Akiwa visiwani Zanzibar katika siku yake ya pili ya ziara ya kikazi, Waziri Ummy ametembelea miradi ya TASAF na MIVARF ikiwa ni pamoja na Kituo cha Afya Kianga, Bwalo la Wanafunzi na Soko la Mbogamboga la Kinyasini.
Amesema
pamoja na changamoto zilizopo zipo fursa kwa Watanzania kujiletea maendeleo na
ustawi wao, kwa kuwa kuwepo kwa fursa hizo kumeleta tashwishi na matarajio
makubwa kwa wananchi katika kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na kuchochea
mafanikio katika maeneo mengine kwa maslahi ya Taifa
“Tumejionea
wenyewe mpango huu mkubwa wa kunusuru kaya maskini kupitia Muungano wetu unatekelezwa na pande zote mbili
na haya ndio matunda ya Muungano kuhakikisha miradi mikubwa inatekelezwa pande
zote mbili” Ummy alisisitiza.
Aimetaja
baadhi ya Miradi ya maendeleo inayotekelezwa na
Serikali zeto mbili yenye kunufaisha
wananchi wake iko katika Nyanja za
Elimu; Afya; Masoko; Maji; Mazingira pamoja na Usafiri na Usafirishaji.
“Kama mnavyofahamu tunataka kuulinda, kudumisha na kuuimarisha
muungano wetu kwani ndio umoja wa
watanzania, ndio usalama wa watanzania na ndio amani ya watanzania wote”
Alisisitiza Mhe. Waziri
Kupitia mradi wa MIVARF takriban masoko 16 yamejengwa Tanzania
nzima kati ya hayo masoko 4 yamejengwa Zanzibar, kituo cha afya Kianga chenye
kunufaisha takriban Shehia 3 za Kianga, Dole na Mazizini huku kikihudumia takribani wakazi 19,840,
ujenzi wa madarasa katika Skuli za Fujoni na Mahonda ambazo zimeweza kutatua
changamoto za elimu.
Waziri
Ummy Mwalimu amesema kuwa ni vyema tukatumia ipasavyo fursa zilizopo Tanzania
Bara na Zanzibar kwa kuleta maendeleo yatakayoinua hali ya uchumi wa
Watanzania, na kutoa rai ya kuulinda, kuuimarisha na kuudumisha Muungano wetu
kwani ni dira ya mafanikio yetu.
Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza la Uwakilishi (Mwera) Mhe. Mihayo Juma N’hunga ameshukuru Serikali kwa kupata kusogeza huduma zenye kugusa Maisha ya wananchi.
No comments:
Post a Comment