Sunday, December 13, 2020

WAKUU WA MIKOA YA MTWARA NA KAGERA WATEMBELEA MIRADI MIKUBWA INAYOTEKELEZWA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO MKOA WA DAR ES SALAAM


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jeneral Marco Gaguti na timu ya Madereva wa Bodaboda kutoka mikoa hiyo miwili leo wamefanya ziara ya kutembelea na kujionea miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkoa wa Dar es salaam.

Katika ziara hiyo wakuu hao wa mikoa na waendesha Bodaboda wamemtembelea Mradi wa Ujenzi wa reli ya kisasa SGR na jengo la abiria la Tanzanite, Mradi wa Mabasi ya mwendo wa haraka, Ujenzi wa stand mpya ya Mabasi ya Mbezi Luis, Daraja la Juu Ubungo na Mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi two.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amesema wameamua kuwaleta waendesha Bodaboda kwenye ziara hiyo ili waweze kujionea Mambo mazuri na makubwa yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano ili wawe mabalozi wazuri kwa wenzao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jeneral Marco Gaguti ameipongeza Serikali kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya Katika utekelezaji wa miradi yenye lengo la kutatua kero kwa wananchi.

Aidha Brigedia Jenerali Gaguti amesema mbali na ziara hiyo Jana pia walifanya mashindano ya Mpira wa moguu kati ya Timu ya Bodaboda Mtwara na Timu ya Bodaboda Kagera kwa lengo kujenga uzalendo kwa kundi hilo la vijana na kuwafanya kuwa mabalozi wazuri wa shughuli za Serikali.

No comments:

Post a Comment