Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula ameungana na wananchi wa Jimbo hilo kusheherekea bonanza la sikukuu ya Christmas na mwaka mpya wa 2021 na kutoa zawadi mbalimbali kwa wananchi waliojitokeza.
Ilemela Christmas Bonanza limefanyika katika viwanja vya Furahisha wilaya ya Ilemela likipambwa na maonesho ya bidhaa tofauti tofauti kutoka kwa wajasiriamali wa mkoa wa Mwanza, mashindano ya kula, kuimba, kucheza, maonesho ya karate na michezo mingine mbalimbali ambapo Mbunge Dkt Mabula akawataka wananchi kusheherekea sikukuu kwa amani, upendo na utulivu huku akiwataka kujiandaa kufanya kazi kwa bidii katika kipindi cha mwaka mpya unaokuja ili waweze kujiletea maendeleo wao wenyewe na taifa kwa ujumla
'.. Nawatakia heri ya sikukuu ya Christmas na mwaka mpya wa 2021 wananchi wote, Kikubwa tusheherekee kwa upendo, amani, utulivu na mshikamano ..' Alisema
Aidha Dkt Mabula akawapongeza waandaji wa bonanza hilo taasisi ya The Angeline Foundation kwa ushirikiano na kampuni ya Coca Cola kwa kazi kubwa waliyoifanya.
Kwa upande wake mwakilishi wa taasisi ya The Angeline Foundation Ndugu Fidelis Lubala akafafanua kuwa bonanza hilo ni mwendelezo wa lile la mwaka Jana na itakuwa ikifanyika hivyo kwa kila mwaka ambapo kwa mwaka huu malengo makuu yalikuwa ni kutoa nafasi kwa wasanii wa Ilemela kuonyesha vipaji vyao, kushukuru wananchi kwa kumchagua na kutoa fursa ya kusheherekea sikukuu pamoja
Kwa niaba ya wananchi wengine waliojitokeza, Bi Prisca Emmanuel Masanja akasema kuwa amefurahishwa na bonanza hilo sambamba na kutaka viongozi wengine kuiga mfano huo wa kutenga muda kukaa na wananchi pamoja ili iwe rahisi kufikisha kero na changamoto zao kwa urahisi.
No comments:
Post a Comment