Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Dkt. Leonard Chamuriho, akisisitiza jambo kwa menejimenti ya Wizara hiyo, mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wizara, jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Godfrey Kasekenya, Kulia ni Katibu Mkuu-Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga.
Naibu Waziri Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya, akisisitiza jambo kwa menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wizara, jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Dkt. Leonard Chamuriho, kulia ni Katibu Mkuu-Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Uchukuzi Gabriel Migire.
Katibu
Mkuu-Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga akiwakaribisha Wizarani Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi, Eng. Dkt. Leonard Chamuriho na Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Eng.
Godfrey Kasekenya, mara baada ya kuwasili ofisini hapo kuanza kazi jijini
Dodoma leo.
Waziri wa
Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Dkt. Leonard Chamuriho amewataka watumishi wa wizara
Ujenzi na Uchukuzi kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi ili kuongeza
ufanisi.
Akizungumza
na menejimenti ya Sekta ya Ujenzi na Uchukuzi mara baada ya kuwasili ofisini
hapo jijini Dodoma ameitaka menejimneti kuunganisha wafanyakazi wa sekta zote kufanya
kazi kwa kuzingatia matokeo yanayopimika.
“Jipangeni
kuhakikisha kuwa Watumishi wote wanafanya kazi kwa umoja na ushirikiano ili
kufikia malengo yanayotarajiwa na Serikali katika kuboresha miundombinu nchini’
amesema Eng. Dkt. Chamuriho.
Amemtaka Katibu
Mkuu-Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga na Kaimu Katibu Mkuu Uchukuzi Gabriel Migire
kuhakikisha miradi yote inayoendelea ujenzi wake unakamilika kwa wakati na
tija.
Kwa upande
wake Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi, Eng. Godfrey Kasekenya ameitaka menejimenti
ya Wizara kuweka ratiba ya mara kwa mara ya kukagua miradi ili kupata taarifa
ya maendeleo na kuchukua hatua mapema kwa miradi yenye changamoto.
Akiwakaribisha Waziri na Naibu Waziri,
Katibu Mkuu Ujenzi amewahakikishia viongozi hao ushirikiano kati yao
menejimenti na watumishi kwa sekta anazosimamia.
Waziri Eng. Dkt. Leonard Chamuriho na Naibu Waziri Eng. Godfrey Kasekenya walikuwa katika kikao cha kwanza cha na menejimenti ya wizara mara baada ya kuteueliwa kuongoza wizara hiyo hivi karibini.
No comments:
Post a Comment