Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya mkoa huo, Dk. Binilith Mahenge akiongoza kikao cha Bodi ya Barabara ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe walipata taarifa za maendeleo ya ujenzi wa barabara mkoani humo kutoka Tanroad na Tarura Desemba 16, 2020 jijini Dodoma.
Dk. Mahenge amezitaka Tarura na Tanroads kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika kwa kupata maoni na ushauri wao kabla ya kuanza ujenzi wa barabara na madaraja katika maeneo yao ili kujenga miradi imara inayozingatia jiongrafia na historia ya eneo husika.
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Happiness Mgalula akisoma ajenda za kikao hicho. |
Mratibu wa Wakala wa Barabara vijijini (TARURA) Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Lusako Kilembe akitoa taarifa kwenye kikao hicho kuhusu mipango ya utekelezaji ya miradi ya barabara za Tarura kufikia hadi Novemba, 2020.
Mhandisi Mwandamizi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Mhandisi Jacob Mukasa akielezea katika kikao hicho , kuhusu manufaa na namna mfuko unavyopanga vipaumbele vya kutoa fedha.
Mhandisi wa Barabara wa Tanroads, Clement Ngirwa akielezea katika kikao hicho, kuhusu utaratibu wa kupandisha hadhi barabara na majukumu ya Kamati ya Kitaifa ya Kupanga Barabara katika Hadhi Stashiki.
Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde akichangia hoja akitaka uwepo utaratibu wa barabara za jamii nazo kutengea fedha kwa ajili ya matengenezo.
Mbunge wa Kondoa Vijijini, Dk. Ashatu Kijaji akichangia hoja wakati wa kikao hicho kwa kuzitaka Tarura na Tanroads kuwa na watalaamu wenye ueledi ili waweze kujenga miradi imara kuiiko wanaojenga miradi ya barabara na madaraja dhaifu ambayo mvua ikinyesha inabomoka kirahisi.
Mbunge wa Chemba, Mohamed Monni, akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota akichangia hoja wakati wa kikao hicho. Kuhoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dk. Fatuma Mganga na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chemba, ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi hiyo, Sambala Said
No comments:
Post a Comment