Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa huo (RCC), akiongoza kikao cha kamati hiyo cha kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo mkoani humo, Desemba 17, 2020. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), wakiwa katika kikao hicho muhimu amacho kinafanyika mara mbili kwa mwaka. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Mafuru akielezea jinsi jiji liliyyojipanga |
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa huo (RCC), ameongoza kikao cha kamati hiyo ambacho kimejadili mambo mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
Kamati hiyo ya ushauri inashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo baadhi ya wakuu wa idara wa ofisi ya mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji wa halmashauri, wabunge, wenyeviti wa halmashauri na baadhi ya viongozi wa taasisi.
Awali wajumbe walithibitisha muhtasari wa mambo yote yaliyopitishwa katika kikao kilichofanyika mwaka jana Desemba 19, 2019
Katika kikao hicho wajumbe walijadili mada mbalimbali zilizowasilishwa za jinsi ya kuboresha sekta ya elimu, sekta ya afya, tathmini ya hali ya chakula na maandalizi ya kilimo msimu wa . 2020/21.
Pia, wajumbe walipitia Mpango wa Bajeti ya mwaka 2019/20 na 2020/21 kufikia Noemba 2020, Mpango wa Bajeti wa mwaka 2019/20 kufikia Novemba 2020 na mwelekeo kwa mwaka 2021/22, mapato ya ndani ya Halmashauri na matumizi kufikia Novemba 2020.
Aidha,wajumbe walipatiwa taarifa ya mwenendo wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 2020, Taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Kamati hiyo ya Wakala kwa Huduma ya Misitu (TFS).
Mkuu wa Mkoa, Dkt. Mahenge ameagiza TFS kuweka utaratibu wa kukagua mara kwa mara mwenendo wa upandaji miti katika halamashauri zote ii kuifanya Dodoma kuwa ya kijani. Mkakati huo uhusishe viongozi wa ngazi zote, wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na viongozi wa mkoa.
Baadhi ya maagizo yaliyotolewa kwenye kikao ni; kuunda Kamati ya Mkoa ya kufuatilia uboreshaji wa elimu ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa Mkoa huo ambao kwa hivi sasa unashika nafasi ya 22 kitaifa.
Dkt. Mahenge amewataka viongozi wote wajenge umoja na ushirikiano kwa kuweka misingi imara ya kudumu ya kuinua kiwango cha elimu ambayo ni ufundishaji bora, usimamizi, ufuatliaji na utawala.
Halmashauri zimetakiwa kuandaa vivutio vya uwekezaji, kutenga maeneo maalumu ya uwekezaji na kuangalia uwezekano wa kupunguza bei ya ardhi kwa wawekezaji na hata ikiwezekana kuingia ubia nao.
No comments:
Post a Comment