Thursday, November 19, 2020

DKT. ABBASI AWATAKA VIONGOZI WA MICHEZO KUANDAA MIKAKATI MIKUBWA KUENDELEZA MICHEZO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa nab Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi akizungumza na Wadau wa Michezo (hawapo pichani),  alipokuwa akifungua warsha ya wadau wa michezo ya kutoa maoni kuhusu Kanuni za Taifa  za Kupinga matumizi na mbinu haramu michezoni (Anti Doping).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa nab Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi akizungumza na Wadau wa Michezo (pichani),  alipokuwa akifungua warsha ya wadau wa michezo ya kutoa maoni kuhusu Kanuni za Taifa  za Kupinga matumizi na mbinu haramu michezoni (Anti Doping).

Mwakilishi wa Tume ya Taifa ya UNESCO Rehema Horda akizungumza katika warsha ya wadau wa michezo ya kutoa maoni kuhusu Kanuni za Taifa  za Kupinga matumizi na mbinu haramu michezoni (Anti Doping).

Mkurugenzi wa Michezo  kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusufu Singo akizungumza katika warsha ya wadau wa michezo ya kutoa maoni kuhusu Kanuni za Taifa  za Kupinga matumizi na mbinu haramu michezoni (Anti Doping).

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, leo Alhamisi, Novemba 19, 2020, jijini Dar es Salaam, amefungua semina ya wadau wa michezo kutoa maoni na kisha kuridhia Kanuni za Kitaifa za Kutekeleza Mkataba wa Kimataifa wa Kupambana na Matumizi ya Dawa za kusisimua misuli na Kuongeza Nguvu Michezoni. 

Akizungumza Katika semina hiyo, Dkt. Abbasi, amewataka wanamichezo wa Tanzania kujiamini kwa kufanya mazoezi na kujiandaa badala ya kutumia dawa za kusisimua  misuli ambazo zimepigwa marufuku duniani katika michezo mbalimbali ambayo Tanzania hushiriki. 

Aidha  amevitaka vyama na mashirikisho ya michezo nchini kuja na mikakati makini ambayo Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, itaona namna ya kuisaidia kwani Mhe Rais ameshatangaza dhamira ya kusaidia sana sekta ya michezo. 

 “ Viongozi wa mashirikisho na vyama vya Michezo mnatakiwa kuwa wabunifu na kuandaa mikakati ya kukuza na kuendeleza michezo nchini, kwa kuwa Serikali iliyoko madarakani chini Rais Magufuli imejitolea kuinua na kuisaidia Sekta ya Michezo”, amesema Dkt.Abbasi. 

Dkt. Abbasi ameongeza kuwa  katika warsha hiyo  alisisitiza kuwa kila kiongozi wa chama cha michezo atimize wajibu wake, kwa kutoa maoni ili kuepusha kero ya wanamichezo kufungiwa kushiriki michezo kwa sababu ya Matumizi ya Dawa za kusisimua misuli na kuongeza nguvu  na kuliletea aibu taifa. 

Kwa upande wa Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Bw.Philbert Bayi aliipongeza Serikali kwa kufanikisha kusainiwa kwa mkataba wa Kupinga matumizi na mbinu haramu michezoni mwaka 2017 na sasa Serikali imetimiza ndoto hiyo ambayo imedumu kwa miaka kumi sasa.

No comments:

Post a Comment