Katika kutoa shukrani na fadhila kwa jamii wanayoihudumia, Benki ya Taifa ya Biashara NBC tawi la Bukoba imetoa msaada wa Saruji tani nne katika kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Igabilo ambayo imeonekana kukumbwa na changamoto hiyo.
Akiongea kabla ya kukabidhi msaada huo jana Novemba 20,mwaka huu katika viwanja vya shule ya msingi Igabilo iliyopo Halmashauri ya wilaya Bukoba, meneja wa benki hiyo tawi la Bukoba Mathias Mhangilwa, amesema kuwa msaada huo ni shukrani kwa wananchi ambao wamekuwa wateja wao hivyo wamewiwa kurudisha kile wanachokipata kama faida.
“Msaada huu ni shukrani kwa jamii yetu tunayoihudumia maana tumekuwa tukifanya hivi mara kwa mara na kwa maeneo mbalimbali kulingana na mahitaji ya eneo husika, hapa katika shule hii upo uhaba mkubwa wa madarasa hivyo tumeona tuchangie ili kusaidia katika ujenzi wa madarasa mapya.” Amesema Mhangilwa.
Ameongeza kuwa baada ya serikali ya awamu ya tano kuanza kutoa elimu bila malipo kumekuwepo na ongezeko la wananfunzi ambalo linapelekea kuwepo kwa upungufu wa madarasa hasa kwenye shule hii hali iliyowapelekea kuchangia katika ujenzi huo.
Kwaupande wake kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Bukoba Babylus Mashauri ameishukuru benk hiyo kwa msaada mkubwa ambao utawawezesha kujenga vyumba viwili vya madarasa ili kuweza kupunguza msongamano wa wananfunzi kwenye vyumba vya madarasa.
Mashauri ameongeza kuwa shule hiyo inawanafunzi 789 huku mahitaji ya vyumba vya madarasa kwa mujibu wa maelekezo ya wizara ya elimu ni vyumba 14 ambapo vyumba vilivyopo ni 9 na mapungufu ni vyumba 5 hali inayopelekea mrundikano mkubwa madarasani.
“Msaada wako huu uliotupatia umeongeza chachu kubwa na sisi kama serikali pamoja na wananchi tutaongeza jitihada kubwa hapa ilituweze kuongeza madarasa mawili katika shule hii, na nitoe wito kwa wadau wengine waige mfano huu wa NBC wa kuisaidia serikali katika kuwaetea maenedeleo na sisi tutapokea msaada wowote utakaotolewa.” Amesema Mashauri.
Mwalimu Deusdelit Ibrahimu ni mwalimu mkuu washue ya msingi Ibosa ambaye ameshukuru msaada uliotolewa na NBC akisema kuwa endapo ujenzi utaanza basi utaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa upungufu wa madarasa katika shue hiyo.
Katika hatua nyingine mwalimu huyo ameongeza kuwa changamoto nyingine kubwa inayowasumbua katika shule hiyo ni upungufu wa matundu ya vyoo vya wanafunzi ambapo mahitaji ni vyumba 35 ambapo matundu yaliyopo ni 11 huku upungufu ukiwa ni matundu 24.
Amesema kuwa mahitaji ya vyoo kwa wananfunzi yanatakiwa kupewa kipaumbele kwasababu ya kulinda afya za wananfunzi kutokana na wingi wao katika shule hiyo pamoja na kutunza mazingira.
No comments:
Post a Comment