Tuesday, October 20, 2020

Wanarukwa wahimizwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia Tanzania Prison dhidi ya Simba SC

Wananchi mkoani Rukwa wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao ya Tanzania Proison inayotarajia kupambana na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom nchini Simba SC katika nyasi za Nelson Mandela Oktoba 22, 2020.

Hamasa hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipotembelea uwanja wa Nelson Mandela ili kujionea maandalizi ya uwanja huo kabla ya kupulizwa kipenga siku ya Alhamisi na kusema kuwa hakika ameridhishwa na maandalizi ya ndani ya uwanja nan je ya uwanja.


Mh. Wangabo alisema kuwa mashabiki siku zote wamekuwa ni mchezaji wa kumi na mbili ndani ya Uwanja na anategemewa kuongeza nguvu ya ushindi kwa kushangilia kwa nguvu zote katika dakika 90 za mchezo na kuongeza kuwa asingependa kuwaona wanarukwa wanaisahau timu yao ambayo imesababisha kuja kwa timu hizo nyingine zote na kushabikia timu ambazo ni wapita njia.


“Nisingependa kuona wanarukwa wanashabikia kwa wingi timu ya Simba, kwasababu timu ya simba ikishinda na nyingine ikaja ikashinda, na nyingine ikaja ikatushinda pia, timu hii itashuka daraja, itakaposhuka daraja hizi timu za Simba, Yanga, Azam na timu nyingine, hazitaonekana tena hapa kwahiyo tutakuwa hatujaitendea haki timu ya Prison, kwahiyo sisi tuishangilie timu yetu kwani hii ndiyo iliyotufanya Simba ije, Azam ikaja na Yanga itakuja na timu nyingine zitakuja,”


Aidha alisema kuwa anaiombea timu ya Tanzania Prison ushindi mbali na kutambua kuwa mpira una matokeo matatu, ya kushinda, kufungwa na sare na kusisitiza kwa washabiki wote wa mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi na kuwathibitishia kuimarika kwa usalama Pamoja na upatikanaji wa huduma zote muhimu kwa washabiki wataofika mjini Sumbawanga kutoka mikoa mimngine.


Kwa upnde wao mashabiki wa pande zote mbili wamejitokeza na kudai kila mmoja kuibuka na ushindi katika mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na wapenzi na wadau wa soka mjini Sumbawanga.


Mmoja wa mashabiki wa Tanzani Prison Patrick linus aliwatahadharisha wanasimba kuacha tabia ya kutembea na matokeo mifukoni na matokeo yake na wasifananishe Sumbawanga na maeneo mengi ambapo wameshakwenda na kuibuka na ushindi.


“’Game’ itakapochezwa Alhamisi, watachezea goli mbili lakini kwasababu ni watu wazima tutawapa nafasi ya kagoli kamoja tu, mi niwaombe tu wanarukwa, wakazi wa manispaa (ya Sumbawanga) tujitokeze kwa wingi, tuwape ‘Support’ Prison nao wafurahi, kamawalihama kutoka huko na kuja huku basi nasi tusiwaangushe,” Alisisitiza.


Naye Daudi Mbwala mshabiki wa timu ya Simba SC alisema kuwa Pamoja na kuikaribisha timu ya Simba na kuitakia ushindi lakini bado wanaiheshimu timu ya Tanzania Prison kwa kuweka makazi yake mjini Sumbawanga.

No comments:

Post a Comment