Thursday, October 22, 2020

Mashabiki wa Tanzania Prison wajinadi kuelekea mechi dhidi ya Simba SC

Mmoja wa Viongozi wa kikundi cha Hamasa cha Timu ya Tanzania Prison Stephen Rheda (aliyesimama) akitoa nasaha za mwisho kwa washabiki wenzie katika kikao cha kujipanga kuelekea mechi dhidi ya Simba SC.

Kikundi maalum cha mashabiki wa timu yenye makazi yake mjini Sumbawanga mkoani Rukwa Tanzania Prison leo hii wamejinadi kuiburuza bila ya huruma mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC katika mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Nelson Mandela Oktoba 22, 2020.


Mashabiki hao wameyazungumza hayo baada ya kikao kifupi walichokutana kwa nia ya kupeana maelekezo mbalimbali ya kuwaji uwanjani Pamoja na kupeana mbinu za ushangiliaji ili kuipa hamasa timu yao iweze kuibuka na ushindi katika uwanja wake wa nyumbani mjini Sumbawanga.


Mmoja wa viongozi wa kikundi hicho Frank Mwasakajole alisema kuwa kikundi hicho ni cha kujitolea kutokana na mapenzi yao dhidi ya timu hiyo ya Tanzania Prison na kusisitiza kuwa katika mchezo huo timu ya Simba ijiandae kwa kichapo.


“Tutakapofika uwanjani kundi hili huwa halikai chini linashangilia mwanzo mwisho, katika kikundi hiki kuna wanahamasa wasiopungua 50, kwahiyo wamejitoa pasipo malipo yoyote mwamejitoa kwaajili ya kuishabikia Tanzania Prison, kwahiyo kesho tunakwenda kwaajili ya kushangilia na tuna uhakika kabisa kwamba kesho tunashinda,” Alisema.

No comments:

Post a Comment