Na Agness Nyamaru.
Waziri wa madini Dotto Biteko amewataka wachimbaji wa madini kujiunga katika kuuza madini kwa uwazi kwani serikali haipo tayari kuona Mtanzania akipunjwa haki yake
Akizungumza wakati wa hafla ya ununuzi wa madini ya Tanzanite kutoka kwa mchimbaji mdogo ,bilionea Saniniu Laizer ,lililopatikana mnamo julai 17 Mwaka huu,Biteko amesema serikali haipo tayari kumpunja Mtanzania haki yake kwani mchimbaji akienda kinyume na sheria hawezi kufanikiwa,kwani mwenye dhana ya kutorosha MADINI hayo hata fanikiwa .
Kwa upande wake waziri wa fedha Philip mpango amesema kuwa katika kuhakikisha huduma za fedha zinapatikana katika eneo husika taasisi zote za fedha zitapatikana katika eneo hilo la machimbo ya Mererani.
Naye billioner Saniniu Laizer amewataka wachimbaji wenzake kuwa wazalendo kwa kuacha kutorosha madini kwani utaratibu wa serikali ni mzuri na unalenga kumfaidisha kila mchimbaji mdogo.
Hata hivyo jiwe hilo lenye uzito wa kilo 6.3317 limenunuliwa na serikali kwa Sh.bilioni 4.846 ambapo katika machimbo ya mererani kuna zaidi ya migodi 170 kwani mnamo 2017 walifanikiwa kukusanya Million 238, huku baada ya ukuta huo walifanikiwa kukusanya Sh Billioni 1.4 ikiwa mwaka 2019 walifanikiwa kukusanya Sh billioni 1.998 ikiwa Ni sawa na billioni 2.
No comments:
Post a Comment