Miundimbinu
ya umeme( kulia) ikionekana imekoma jirani na kijiji cha ambacho bado
hakijafikiwa na mradi wa REA,Waziri wa Nishati,Dkt. Medard Kalemani aliigiza
TANESCO, kupeleka umeme katika vijiji vya aina hii, wakati alipofanya ziara ya
kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini katika Wilaya za Nyang’hwale,
Geita na Chato mkoani Geita, Mei 15, 2020.
Muonekanao
wa miundombinu ya umeme inayopita katika baadhi ya vijiji mbacho havina umeme
ama vipo jirani na miundombinu ya umeme na hakijafikiwa na Mradi wa REA, Waziri
wa Nishati,Dkt. Medard Kalemani aliigiza TANESCO, kupeleka umeme katika vijiji
vya aina hii, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa
umeme vijijini katika wilaya za Nyang’hwale, Geita na Chato mkoani Geita, Mei
15,
Waziri wa
Nishati,Dkt. Medard Kalemani( katikati) akizungumza na mwanakijiji wa Izunya,(
kushoto) ambacho kikokaribu na miundombinu ya umeme ambapo aliigiza TANESCO,
kupeleka umeme katika vijiji vya aina hii ambavyo vimepitia au vipo karibu na
miundombinu ya umeme ambavyo havijafikiwa na REA, alipofanya fanya ziara ya
kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme
vijijini katika Wilaya za Nyang’hwale, Geita na Chato mkoani Geita, Mei
15,2020.
Waziri wa
Nishati,Dkt. Medard Kalemani ( kushoto) akizungumza katika kituo cha afya cha
Nyang’hwale alipofika kuwasha umeme katika zahanati hiyo wakati wa ziara ya
kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini katika Wilaya za Nyang’hwale,
Geita na Chato mkoani Geita, Mei 15,2020.
Waziri wa
Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema Mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) watakaoshindwa kutimiza malengo ya kuunganisha umeme vijijini na
kuwawashia wananchi umeme watachukuliwa hatua kwa mujibu wa mikakati iliyowekwa
katika kupima utendaji kazi wao.
Dkt.
Kalemani alisema hayo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme
vijijini ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea baadhi ya vijiji ambavyo
vimepitiwa na vilivyojirani na miundombinu ya umeme ambavyo bado havijafikiwa
na mradi wa usambazaji wa umeme vijijini REA katika Wilaya ya Nyang’hwale,
Geita na Chato mkoani Geita, Mei 15, 2020.
Baada ya
kukagua vijiji hivyo aliwaagiza Mameneja wa TANESCO nchini kuunganisha umeme
katika vijiji hivyo pamoja na kuwawashia wananchi umeme kwa gharama ya shilingi
27,000 tu.
Dkt.
Kalemani aliweka wazi kuwa katika kutimiza azma na malengo ya serikali ya
kuhakikisha kuwa vijiji vyote nchini vinapata umeme, mameneja wa TANESCO kote
nchini waliwekewa vigezo vitatu vya kuwapima na kufanya tathmini ya utendaji
kazi wao katika kutekeleza malengo hayo, zoezi hilo lilianza mwezi Julai, 2019,
ambapo sasa utekelezaji wake unaanza kwa kuwachukulia hatua mameneja hao.
Vilevile
mameneja walitakiwa kuunganisha umeme katika vijiji ambavyo vimepitiwa na njia
ya kusafirisha umeme mkubwa ambavyo bado havijafikiwa na REA pamoja na vile
vilivyo umbali mfupi kutoka katika maeneo yaliyopitiwa na njia za umeme.
Alitaja
tathmini zinazotumika kuwapima mameneja katika utendaji kazi wao, kuwa ni
kuongeza idadi ya wateja katika maeneo yao na kuunganisha wateja hao kwa wakati
mara tu baada ya mteja kulipia gharama za uunganishaji, tathmini hiyo
inachukuwa 45% ya utendaji kazi wake.
Aidha
Mameneja hutathminiwa kwa kutoa huduma bora kwa wateja, hii inatokana na baadhi
ya mameneja kutokuwa na ushirikiano na wateja katika maeneo yao, pia
kutokupokea simu za wateja wala wa kusikiliza kero na kutatua changamoto zao,
hii inachukuwa 20% na Tatu ni kukatika kwa umeme mara kwa mara bila sababu wala
kutoa taarifa kwa wateja katika eneo lake ambalo huchukuwa 30% ya tahmini yake.
“Kama
unakataa wateja katika eneo lako, umeme unakatika mara kumi kwa mwezi,
huwasikilizi wateja wala kutatua kero zao,hupokei simu za wateja wewe hutoshi
na hufai kuwa maneja andika barua ujitoe mwenyewe, pia tunakutoa, mameneja wa
kanda simamieni hili na muanze kuchukuwa hatua, na kama hamtachukuwa hatua
tutaanza kuwatoa kuanzia chini mpaka juu” alisisitiza Dkt. Kalemani.
Aidha
alifanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi Ndogo ya TANESCO ya Katoro na kumtaka
meneja wa kituo hicho kuandika barua ya kujieleza, kutokana na baadhi ya
watumishi wa ofisi hiyo kutokuwepo kazini bila taarifa yoyote, na wengine
kukutwa wakipiga soga bila kuwepo katika maeneo yao ya kazi.
Vilevile
ofisi hiyo haikuwa alama au vibao vinavyomuelekeza mteja katika dirisha husika
la kutolea huduma kama vile eneo la mapokezi, mhasibu na meneja wa kituo.
Kuafuatia
hali hiyo alizataka ofisi za TANESCO nchi kote kuendeshwa kwa kuzingatia
nidhamu za kazi,pia watendaji waache kufanya kazi kwa mazoea kwa lengo la kutoa
huduma bora wateja.
“Hii ni
ofisi ya TANESCO kweli!hakuna alama inayoonyesha sehemu ya mapokezi, kwa
mhasibu wala meneja, nimekuja hapa mpaka naingia ndani hakuna hata wa
kunipokea, sasa mimi ni Waziri, je akija mwananzengo( mwananchi) atapata huduma
kweli! Waliopo ofisi wale kule wanapiga soka wanaacha kukaa sehemu zao
kazi!mchora michoro yuko wapi na wengine je! Meneja unaendesha ofisi kwa mazoea
eee nataka maelezo la sivyo….!”, alifoka Dkt. Kalemani.
Akiwa
katika Wilaya ya Nyang’hwale, Dkt. Kalemani aliwasha umeme katika kituo cha
afya katika eneo hilo, kukagua usambazaji wa umeme katika kijiji cha Izunya na
na kuwagiza TANESCO kupelekea umeme katika vijiji hivyo ambavyo vipo karibu na
miundombinu ya umeme na havijafikiwa na mradi wa REA kwa awamu zilizotngulia.
Katika
Wilaya ya Geita aliagiza kuunganisha umeme katika kijiji cha Shinamwendwa
kilichopitiwa na njia ya kusafirisha umeme mkubwa na kijiji cha Chibingo
ambavyo vyote hakijafikiwa na mradi wa REA, na katika wilaya ya Chato aliwasha
umeme katika moja ya kanisa katika
kijiji cha Buzirayombo na kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Buseresere na
kuagiza TANESCO kupeleka umeme katika kituo hicho ili kuharakisha ujenzi wa
kituo hicho.
Katika
hatua nyingine alimtaka mkandarasi anayetekeleza usambazaji wa umeme vijijini
katika Wilaya ya Nyang’hwale kukamisha kazi ya kuwasha vijiji vilivyosalia na
akishindwa kufanya hivyo atakatwa 10% ya malipo yake na kuchukulia hatua za
kisheria kwa kuchelewesha huduma kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment