Afisa Utumishi wa Shamba la Miti Sao Hill Felista Bayo akikabidhi msaada huo kwa msimamizi wa kituo cha watoto yatima cha SISI NI KESHO
Picha ya watoto yatima na wafanyakazi wa kituo cha watoto yatima cha SISI NI KESHO wakiwa na baadhi ya wafanyakazi wa shamba la miti la Sao Hill Mufindi
NA FREDY MGUNDA,MUFINDI.
Wadau mbalimbali wametakiwa
kuendelea kuwachangia na kuwakumbuka Watoto wenye mahitaji maalumu na yatima
kwa lengo la kuwafariji kwa kuwasaidia kupata mahitaji yao muhimu kama ambavyo
familia nyingine zinapata majumbani yao.
Akizungumza kwa niaba ya
watumishi wanawake wa Shamba la Miti Sao Hill,Afisa Utumishi wa Shamba la Miti
Sao Hill Felista Bayo alisema kuwa watanzania wanatakiwa kuwa na moyo wa
kujitolea kusaidia Watoto ambao hawana uwezo na wale yatima ili nao watimize
malengo yao.
Alisema kuwa Baadhi ya watumishi
wanawake kutoka TFS - Shamba la Miti Sao Hill wamekuwa wakijitolea kusaidia Watoto
yatima mara kwa mara kwa lengo la kuifanya jamii nyingine kuiga mfano huo wa
kusaidia Watoto.
Bayo alisema kuwa Vifaa walivyokabidhiwa
ni sukari, mchele mafuta ya kupikia na kupaka, sabuni , pampers, kandambili,
chumvi, track suit, sweta, juice, biscuits, blanketi, unga wa lishe na mahindi
kwa kuwa hayo ndio mahitaji ya Watoto hao.
“Tulitembelea kwanza kituo hicho
na kujua mahitaji ambayo yanahitajika na kuyatafuta ndio maana tulipeleka mahitaji
hayo kulingana na mahitaji ya kitu cha Watoto yatima cha SISI NI Kesho kilichopo
katika kijiji cha Nyololo Wilayani Mufindi katika Mkoa wa Iringa” Bayo
Bayo alisema kuwa vifaa vinavyokabidhiwa
vina thamani ya shilingi laki sita sitini na moja elfu (Tsh 661,000/=) ambapo fedha
hiyo imechangwa na wanawake wafanyakazi wa shamba la miti ya Sao Hill
Naye Msimamizi wa kituo hiko Bi. Jane Mkondola ametoa wito kwa wadau wengine kuendelea kuchangia kituo hiki na watu wengine wenye mahitaji ili kuwezesha malezi ya watoto kuwa mazuri zaidi kwani lengo la kituo hiki sio kujipatia faida bali ni kutoa huduma.
Watumishi wanawake TFS - Shamba la Miti Sao Hill wamekuwa wakisaidia vituo vya watoto yatima Kila mwaka ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani.
No comments:
Post a Comment