Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akizungumza kwenye ziara ya Iringa mpya awamu ya pili alipokuwa anakagua ujenzi wa barabara yaKinyanambo, Pareto,Chumi,Lutherani na Mwamkoa Mbagala iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga akiwataka wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA) kusitisha ujenzi wa barabara hizo kwa kuwa ujenzi huo hauna tija kwa wananchi
Baadhi ya uharibifu unaondelea kwenye maeneo ambayo ujenzi wa barabara unaendelea hivi sasa kwenye maeneo ya Mji wa Mafinaga Mji.
Baadhi ya uharibifu unaondelea kwenye maeneo ambayo ujenzi wa barabara unaendelea hivi sasa kwenye maeneo ya Mji wa Mafinaga Mji
NA FREDY MGUNDA,MUFINDI.
SERIKALI ya mkoa wa Iringa imewataka
wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA) kusitisha ujenzi wa barabara za
vumbi zinazoendelea kujengwa na wakandarasi mbalimbali kutokana mvua kubwa
zinazoendelea hivi sasa.
Akizungumza kwenye ziara ya
Iringa mpya awamu ya pili alipokuwa anakagua ujenzi wa barabara yaKinyanambo, Pareto,Chumi,Lutherani
na Mwamkoa Mbagala iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga,mkuu wa mkoa wa
Iringa Ally Hapi aliwataka wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA)
kusitisha ujenzi wa barabara hizo kwa kuwa ujenzi huo hauna tija kwa wananchi.
Kipindi hiki mvua zinanyesha
kwa wingi kila kona na zimekuwa zikiharibu miundombinu katika maeneo mengi
katika mkoa huu wa Iringa,hivyo kutokana na hali hiyo natangaza kusitisha
ujenzi wa barabara hizo hadi pale mvua zitakapo isha.
Hapi aliwataka viongozi wa
TARURA kuhakikisha wanawasimamia vilivyo wakandarasi wote wanajenga barabara
hizo ili zijengwe katika ubora unatakiwa kulingana na thamani ya fedha
iliyotolewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
“Hakikisheni mnawasimamia
vilivyo wakandarasi hao kwa kuwa fedha zinazotumika ni kodi za wananchi hao
ambao mnawaona hapa,hivyo lazima thamani ya fedha hizo ionekane kwa wananchi
hawa” alisema Hapi
Hapi aliwataka TARURA kuongeza
kasi ya ujenzi wa mitandao ya barabara za lami katika Halmashauri ya Mji wa
Mafinga na ujenzi wa taa za barabarani ili Halmashauri ya Mji wa Mafinga kuwa
Manispaa na hatimaye mkoa wa Iringa kuwa Jiji.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya
ya Mufindi Jamhuri Wiliamu aliwataka TARURA
kujenga mitaro yenye ubora unaotakiwa ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa
inamudu maji yote yanayopita na kuzilinda barabara zisiaharibike haraka na
zidumu kwa muda mrefu.
“Barabara zetu nyingi za wilaya
hii zinaharibika kutokana na kutokuwa na mitaro iliyobora inayohimili maji
mengi na ndio maana barabara zinaharibika kila uchwao hizi ni bora kuweni
wakali kwa wakandarasi wanaopewa tenda za mitaro kwenye barabara husika”
alisema Wiliam
Akijibia hoja za mkuu wa
mkoa,mwananchi Inocent Mahanga na mkuu wa wilaya ya Mufindi,meneja wa TARURA
Mafinga Tc Injinia Simoni Ngagani alisema kuwa watahakikisha barabara
zinajengwa kwenye ubora unatakiwa kulingana na thamani ya fedha za mradi
husika.
Tutahakikisha ujenzi wa
Mifereji na barabara zinajengwa kwa viwango stahili ili kutumia vilizuri kodi
za wananchi.
No comments:
Post a Comment