Monday, March 2, 2020

MBUNGEWA JIMBO LA WAWI KWA TIKETI CUF AOMBA KUJIUNGA NA CCM – PEMBA



MBUNGE wa jimbo la wawi kwa tiketi Cuf aomba kujiunga na Ccm – Pemba


katika ziara ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba Zanzibar Ndugu Humphrey Polepole Katibu Mwenezi wa CCM Taifa amepokea maombi ya Mbunge wa Jimbo la Wawi kwa tiketi ya CUF kuomba kujiunga na CCM.
Hatua hiyo imekuja baada ya Ndugu Ahmed Juma Ngwali kuusimamisha msafara wa Ndugu Polepole, kuomba kujiunga na CCM na kutangaza kujivua nafasi zake zote ndani ya Chama cha CUF.
Aidha Ndugu Ahmed Juma Ngwali amepokelewa na Ndugu Polepole katika iliyokuwa ngome ya CUF ya Semewani akiambatana pamoja na Wanachama 1895 wa Chama cha CUF na ACT Wazalendo. 
Ziara ya kufuatilia na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM imeendelea kisiwani Pemba Wilaya ya Chakechake kwa kutembelea na kukagua kisima cha Maji safi na salama Chanjaani, Mashamba ya Mpunga katika bonde la Dobi, Ujenzi wa Bohari ya madawa, Kituo cha Afya Mbuzini, Ujenzi wa Skuli ya awali ya Mavungwa na barabara ya Michungwani

No comments:

Post a Comment