Mawaziri wa Sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao ni Mhe.Mahmoud Thabiti Kombo (katikati),Mhe.Harrison Mwakyembe (kushoto) na kulia Mhe.Balozi Ally Abeid Karume wakisaini taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya kikao cha maeneo ya ushirikiano kati ya Serikali hizo kilichofanyika mwezi julai 2019 jijini Dodoma,Taarifa hiyo wameisaini visiwani Zanzibar machi 04,2020.Wanaoshuhudia ni Manaibu mawaziri pamoja na Makatibu Wakuu wa sekta
hizo.
Mhe.Mahmoud Thabiti Kombo Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya kale SMZ (katikati) akiongoza kikao cha kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika kikao cha mawaziri kilichofanyika julai,2019 jijini Dodoma pamoja na mapendekezo ya maeneo mapya ya ushirikiano baina ya Wizara zenye dhamana ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo SMT na SMZ kilichofanyika Zanzibar machi 04,2020.Kushoto ni Mhe Harrison Mwakyembe Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo (SMT) na kulia ni Mhe.Balozi Ally Abeid Karume Waziri wa Vijana, Utamaduni,Sanaa na Michezo (SMT).
Mhe.Juliana Shonza Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo akichangia mjadala katika kikao cha kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika tarehe 02,julai 2019 jijini Dodoma pamoja na mapendekezo ya maeneo mapya ya ushirikiano baina ya Wizara zenye dhamana ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo SMT na SMZ kilichofanyika Zanzibar machi 04,2020.
Mhe.Chum Kombo Hamis Naibu Waziri Habari,Utamaduni na Mambo ya kale akichangia mjadala katika kikao cha kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika tarehe 02,julai 2019 jijini Dodoma pamoja na mapendekezo ya maeneo mapya ya ushirikiano baina ya Wizara zenye dhamana ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo SMT na SMZ kilichofanyika Zanzibar machi 04,2020.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimekubaliana kuboresha kombe la Mapinduzi ili liwe na sura ya Muungano kwa kuhakikisha mfumo wa uendeshaji wa kombe hilo unafuata taratibu za muungano pamoja na kutumia wachezaji wenye sifa ambazo zinatumika katika ligi nyingine.
Makubaliano hayo yamefikiwa jana visiwani Zanzibar katika katika kikao cha kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika tarehe 02,julai 2019 jijini Dodoma kilichokua na lengo la kubainisha maeneo ya ushirikiano pamoja na kujadili mapendekezo ya maeneo mapya ya ushirikiano baina ya Wizara zenye dhamana ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo SMT na SMZ.
Katika kikao hicho Mwenyekiti Mhe.Mahmoud Thabiti Kombo Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya kale SMZ amesema kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha Muungano unalindwa na unaenziwa katika nyanja mbalimbali ambazo zinakubalika baina ya pande mbili hivyo kombe la Mapinduzi linapaswa kuwa na ushawishi mkubwa kama ilivyokua kombe la Muungano ambalo lilikuepo huko nyuma.
“Kwa mujibu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe,Dkt. Ally Mohamed Shein Wizara zetu ni miongoni mwa Wizara zinazoshirikiana vizuri katika kutekeleza maazimio ya maeneo ya muungano kama yalivyoelekezwa na ofisi ya Makamu wa Rais hivyo tuendelee kufanya hivyo” alisema Mhe.Mahmoud.
Kwa upande wake Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe amesema kuwa muungano ni suala la lazima na ni utamaduni wetu hivyo kila mtanzania anapaswa kuulinda ambapo amesema kuwa jukumu la serikali ni kuweka mikakati imara ya kutekeleza hilo kama ambavyo imefanya katika matamasha mbalimbali kama ZIFF,Sauti za Busara,Zanzibar Cultural Festival,Urithi Festival, Tamasha la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambayo yanatoa fursa kwa watanzania kutangaza bidhaa za sanaa na kutafuta masoko.
“Ni lazima pia tushirikiane katika kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali zetu kwa wananchi ili wawe na uelewa wa kutosha juu ya nchi yao hivyo idara za Habari zinapaswa kushrikiana kwa karibu zaidi”alisema Dkt.Mwakyembe.
Hata hivyo kikao hicho kiliagiza BAKITA na BAKIZA kutumia Balozi za nchi yetu kuwezesha wataalam wa uandishi wa habari kupata fursa za ajira katika vyombo vya habari vya kimataifa ili kukuza lugha ya Kiswahili nje ya nchi.
Vilevile kikao hicho kilisistiza waandaji kutumia muongozo wa vikao vya ushirikiano uliotolewa na ofisi ya Makamu wa Rais (SMT) ambao umesambazwa katika Wizara hizo tatu ili kuwa na mfumo unaotambulika.
No comments:
Post a Comment