Wednesday, February 19, 2020

WAZIRI HASUNGA ATANGAZA KUSHUKA KWA BEI YA MBOLEA YA KUKUZIA (UREA)

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa mbolea nchini, hafla iliyofanyika Jijini Dar es slaam leo tarehe 19 Februari 2020. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kutoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa mbolea nchini, hafla iliyofanyika Jijini Dar es slaam leo tarehe 19 Februari 2020.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa mbolea nchini, hafla iliyofanyika Jijini Dar es slaam leo tarehe 19 Februari 2020.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kutoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa mbolea nchini, hafla iliyofanyika Jijini Dar es slaam leo tarehe 19 Februari 2020.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Katika msimu wa kilimo 2018/19 wastani wa bei za mbolea aina ya Urea nchini ilikuwa Tshs 57,500/= kwa mfuko wa kilo 50.

Kutokana na tafiti mbalimbali zilizolenga katika kutafuta namna ya kupunguza bei hizo ikiwa ni pamoja na uingizaji wa mbolea kupitia zabuni za ushindani zinazosimamiwa kupitia mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (BPS – Bulk procurement System), bei za mbolea aina ya UREA imepungua hadi wastani wa Tshs 51,700/= ambayo ni sawa na punguzo la asilimia 10 kwa mfuko wa kilo 50.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 19 Februari 2020 wakati akitoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa mbolea mbele ya waandishi wa habari Jijini Dar es slaam.

Mhe Hasunga amesema kuwa bei ya mkulima imepungua kwa wastani Kimkoa kutoka Tshs 54,000/= kwa mwezi Julai 2019 hadi wastani wa Tshs 51,700/= kwa mwezi Novemba 2019. Hilo ni punguzo la wastani wa Tshs 2,300/= au asilimia 4 kwa mfuko wenye uzito wa kilo 50.
Kuhusu hali ya upatikanaaji wa mbolea Mhe Hasunga amesema kuwa katika msimu wa 2019/2020, mahitaji ya mbolea ni tani 586,604. Hadi kufikia Februari 18, 2020 upatikanaji wa mbolea ulifikia tani 491,659 sawa na asilimia 84 ya mahitaji ya nchi.
Kati ya mwezi Julai 1, 2019 na Februari 18, 2020 jumla ya tani 17,832 za mbolea (Fertilizer) na visaidizi vya mbolea (Fertilizer supplements) zilitengenezwa hapa nchini; ambapo tani 17,157 zilikuwa za mbolea zilizotengenezwa na Kampuni ya Minjingu na Kampuni zingine 10.
Tani 675 zilikuwa za visaidizi vya mbolea vilivyotengenezwa na Kampuni za ABM ya Tanga. Aidha, jumla ya tani 305,729 za aina mbalimbali za mbolea ziliingizwa nchini; ambapo tani 94,325 ni za mbolea ya Urea na tani 57,410 ni DAP; sawa na asilimia 50 ya mbolea zote zilizoingizwa nchini.
Waziri Hasunga amesema kuwa kuanzia julai 2019 hadi 18 februari 2020 upatikanaji wa urea ni tani 136,163 na DAP tani 100,720. Mbolea zingine zilizoingizwa ni pamoja na NPK, SA, CAN, MoP na mbolea zingine ambazo kwa sehemu kubwa ni zile zenye nyongeza za virutubisho (Micronutrients) ambazo husaidia kuboresha ukuaji wa mazao, kuzuia upotevu wa virutubisho kutokana na kuchukuliwa na maji (leaching) na/au kuongeza muda wa mazao kutunzwa kabla ya kuharibisha (perishability).
Aidha, zaidi ya tani 70,000 zikiwemo tani 8,800 za DAP na tani 58,357.254 za Urea zinatarajiwa kuingia nchini ndani ya juma la tatu la Mwezi Februari, 2020. Hilo litafanya jumla ya upatikanaji wa mbolea kuwa zaidi ya asilimia 100 ya mahitaji ya nchi na hivyo kuhakikisha uwepo wa mbolea za kutosha nchini hadi kufikia mwisho wa msimu wa kilimo 2019/20.
Hasunga ameeleza kuwa Mbolea ya kukuzia ya Urea iliwasili nchini Januari 24, 2020 na imekwishapakuliwa na tayari imesambazwa mikoani. Hivyo, bei elekezi katika maghala ya Dar es salaam (DSM ex-warehouse price) itakuwa Tshs 43,104/= kiasi cha mbolea kisichopungua tani 30 zikinunuliwa kwa pamoja. Aidha, bei za jumla zitapatikana katika kila kituo cha mauzo kwa kiasi cha mbolea kisichopungua tani 5 zikinunuliwa kwa pamoja.
Bei elekezi ya rejareja kwa mkulima kwa mbolea aina ya Urea kwa mikoa ya Kanda ya Mashariki, Kati, Kusini na Kaskazini zitakuwa kati ya Sh. 44,800/= na 53,400/=. Kwa mikoa ya Kanda ya Magharibi, Nyanda za Juu Kusini na Ziwa, bei elekezi kwa mbolea aina ya urea itakuwa kati ya Sh. 50,000/= na 57,300/=.
Waziri Hasunga amesema kuwa bei hizo zitaanza kutumika rasmi tarehe 20 Februari, 2020 na zitaendelea kutumika hadi pale itakapotangazwa bei nyingine.
Ikumbukwe kwamba hizi ni bei za ukomo wa juu (Ceiling prices) katika ngazi za bei ya ghalani, jumla na ya Mkulima katika eneo husika. Hivyo wafanyabiashara wanaweza kuuza chini ya bei elekezi bila kuathiri ubora wa mbolea. Kwa kuzingatia hilo, Wizara imetoa bei elekezi ya jumla na rejareja za mbolea kwa uzani wa kilo 50, 25, 10 na 5 katika kila kituo cha mauzo. Aidha, izingatiwe kuwa ni kosa kisheria kuuza mbolea kwa bei ya juu ya bei kikomo kwa nia ya kujiongezea kipato” Alikaririwa Mhe Hasunga
Kadhalika amesema kuwa endapo kutakuwa na tofauti ya gharama za usafirishaji katika baadhi ya maeneo ambayo itakuwa haiendani na bei elekezi, amewaagiza Wakuu wa Mikoa/Wilaya kukaa na Kamati za pembejeo na kurekebisha bei hizi ili ziendane na hali halisi ili kuwezesha usambazaji na upatikanaji wa mbolea kwa wakulima.
MWISHO

No comments:

Post a Comment