Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akikagua na kutoa maelekezo ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji wa Tabora, Igunga, Nzega na Uyui
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (katikati) akipokea maelezo ya ujenzi wa mradi kutoka kwa Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa mradi wa maji wa Tabora, Igunga, Nzega na Uyui wakati wa ziara yake kwenye mradi huo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akitoa maelekezo kwa wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa maji wa Tabora, Igunga, Nzega na Uyui wakati wa ziara yake kwenye mradi huo.
Ujenzi ukiendelea kwenye moja ya eneo la mradi wa maji wa Tabora, Igunga, Nzega na Uyui
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji
Mhandisi Anthony Sanga amewataka wakandarasi wanaojenga mradi wa maji wa
Tabora, Igunga, Nzega, Uyui na Tabora kuongeza kasi ya utekelezaji wake ili ukamilike
kwa wakati.
Mhandisi Sanga ametoa maelekeo
hayo Mkoani Tabora Februari 4, 2020 wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji
wa miradi mbalimbali ya maji mkoani humo.
Mara baada ya kutembelea eneo la
mradi huo na kujionea hatua iliyofikiwa, Mhandisi Sanga alizungumza na
wakandarasi wanaoutekeleza ambapo alieleza kuridhishwa kwake na hatua
iliyofikiwa.
Hata hivyo, licha ya kuridhishwa
na ubora wa ujenzi wa mradi, Mhandisi Sanga aliwataka wakandarasi hao kuelekeza
nguvu zaidi kwenye kazi zinazopelekea wananchi kupata maji kwanza badala ya
kuweka nguvu kubwa kwenye maeneo mengine.
“Pamoja na kazi nzuri
inayoonekana kufanyika maaelekezo yangu ni kuwa wakandarasi wote mhakikishe
kuwa kazi zinazofanyika kwa sasa ni zile ambazo wananchi wataanza kupata maji
mapema iwezekanvyo badala ya kuweka nguvu kwenye majengo na mambo mengine,“
alisisitiza Mhandisi Sanga.
Alibainisha kuwa wananchi
wamesubiri mradi huo kwa muda mrefu na kwamba kwakuwa tayari kumefanyika kazi
kubwa wahakikishe maeneo machache ambayo bado hayajakamilika
wanayakamilisha.
“Mnapaswa kuelewa wananchi
wameusubiri mradi huu kwa muda mrefu, hizi kazi zilizobakia mhakikishe
zinakamilika haraka, shughuli zingine kama kupaka rangi majengo zitafanyika
baada ya kuwa tayari wananchi wanapata huduma,” aliongeza Mhandisi Sanga.
Kwa upande wao Wakandarasi hao
walimhakikishia Naibu Katibu Mkuu kutekeleza maelekezo aliyoyatoa na waliahidi
kuhakikisha wanaongeza kasi ya ujenzi wa mradi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi
hadi muda wa ziada ili tu inapofika Februari mwishoni maji yawe yamefika kwenye
maeneo yote yaliyokusudiwa ya Tabora mjini, Nzega, Igunga na Uyui.
Mradi wa maji wa Tabora, Igunga,
Nzega na Uyui unajengwa na Kampuni tatu kutoka India ambazo ni Megha
Engineering Infrastructures, L&T na Afcons kwa gharama ya shilingi
Bilioni 602 zikiwa ni fedha za mkopo kutoka benki ya Exim ya India.
Mradi huo unatekelezwa kwa
kipindi cha miezi 30 kutoka Agosti 2017 na unatakiwa kukamilika tarehe 23
Februari, 2020 kwa mujibu wa mkataba na kwamba kukamilika kwake kutawezesha
jumla ya wananchi 1,200,000 kunufaika na huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria.
No comments:
Post a Comment