Tuesday, February 4, 2020

TTB YAPANIA SOKO LA UTALII UINGEREZA, YAMKABIDHI RASMI UBALOZI WA UTALII NICK REYNALD “BONGOZOZO”


Meneja Masoko kutoka Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Meena akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), katika hafla fupi ya kupewa Ubalozi wa Utalii wa Tanzania nchini Uingereza kwa bwana Nick Reynald ‘Bongozozo’ iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, leo Februari 04, 2020, kulia ni Afisa Uhisiano Mkuu TTB, Geofrey Tengeneza na kushoto ni Balozi wa hiari wa Utalii wa Tanzania nchini Uingereza, Bw. Nick Reynald ‘Bongozozo’ 
Balozi wa hiari wa Utalii wa Tanzania nchini Uingereza, Bw. Nick Reynald ‘Bongozozo’ akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), katika hafla fupi ya kupewa Ubalozi wa Utalii wa Tanzania nchini Uingereza iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, leo Februari 04, 2020, kulia ni Afisa Uhisiano Mkuu TTB, Geofrey Tengeneza na kushoto ni Meneja Masoko kutoka Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Meena 
Meneja Masoko kutoka Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Meena(kushoto) akimkabidhi jarida la utalii (Tanzania Unforgetable) Bw. Nick Reynald ‘Bongozozo’(katikati)  aliyekabishiwa barua rasmi kuwa balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania nchini Uingereza,  kulia ni Afisa Uhisiano Mkuu TTB, Geofrey Tengeneza 
Meneja Masoko kutoka Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Meena(kushoto) akimkabidhi FLASH yenye video za utalii wa Tanzania  balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania  Bw.Nick Reynald ‘Bongozozo’(katikati)  aliyekabishiwa barua rasmi leo Februari 04,2020, kulia ni Afisa Uhisiano Mkuu TTB, Geofrey Tengeneza.
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii nchini (TTB), leo imetekeleza agizo la Waziri wa Wizara hiyo, Dkt.Hamisi Kingwala alilolitoa Jijini Dodoma jana Februari 03,2020 la kumpa Mwingireza Nick Reynald maarufu kama Bongozozo ubalozi wa utalii wa Tanzania nchini Uingireza.

Akizungumza katika hafla ya kumkabidhi barua ya utambuzi kwa ajili ya kazi hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa TTB, Geofrey Meena alisema kuwa, Nick Reynald aliyezaliwa Zimbabwe na kuishi Tanzania kwa miaka 18 yaani tangia mwaka 1998 atakuwa balozi mzuri kwa uitalii wa Tanzania kwa sababu maeneo mengi ya utalii anayajua.

“Nick Reynald ‘Bongozozo’ ameishi hapa nchini kwa miaka mingi kuanzia mwaka 1998 mpaka sasa ni miaka 18 kwa hiyo anauelewa na utalii wa Tanzania, amekuwa maarufu sana hapa nchini kutokana na  mapenzi makubwa kwa Tanzania ambayo yemejidhihirisha katika nyanja nyingi ikiwemo ushabiki wa mpira kwa timu ya Taifa ‘Taifa Stars” pamoja na wachezaji akiwemo Mbwana Samatta anayekipiga kunako klabu ya mpira ya Astoni villa nchini Uingireza”, Alisema Geofrey Meena.

No comments:

Post a Comment