Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mh. RITTA KABATI ametoa msaada wa Saruji Tani 1 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Mtwivila.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Msaada huo Mbunge KABATI amesema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuhakikisha wanafunzi wa shule ya Msingi mtwivila wanasoma katika mazingira rafiki yatayosaidia Kuongeza ufaulu.
“hawa watoto tukiwatengenezea mazingira rafiki shuleni hata ufaulu utaongezeka. Sasa hivi Iringa Inafanya vizuri katika elimu, tusirudi nyuma tutengeneze mazingira sasa tuzidi kung’ara katika elimu ngazi zote”
Aidha Mh. KABATI amewataka wananchi wa Mtwivila kuuunga Mkono juhudi za kukuza sekta ya elimu kwa kushirikiana na wadau ambao wamekuwa wakisaidia katika ujenzi wa Miundombinu ya shule.
“watoto hawa sio wa serikali tu bali ni watoto wa kwetu na serikali. Hivyo tukiona kuna vitu vimechelewa kidogo sisi kama wazazi tuungane tuboreshe kilichopungua kwa sababu watatusaidia baadae wakipata elimu bora”
Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika zoezi la ugawaji wa Msaada huo, Bwa. CHRISTOPHER PALANJO ambaye ni katibu wa CCM iringa Mjini amempongeza Mbunge RITTA KABATI kwa kutoa msaada huo huku akiwataka wadau wengine kuwa na moyo wa kuchangia katika sekta ya elimu.
“Mama Ritta Kabati anatutoa uyatima wanaIringa, kwa sababu ya kutokuwa na mbunge wa jimbo yeye ameshika nafasi hiyo kwa mkoa wa Iringa na anatutendea haki kwa juhudi zake katika kila sekta”
Naye Mwenyekiti wa Mtwivila A Bw. Boniface Magesa amewataka watendaji wote wa mtaa huo kuitumia mifuko hiyo kwa kwa ajili ya ujenzi wake ili kukaribisha zaidi wadau wengine wa maendeleo katika kata hiyo.
“sisi wakazi wa Mtwivila tunakushukuru sana kwa msaada wako wa mifuko hii ya saruji, tunakuomba utusaidie tena kutupatia wadau wa maendeleo katika mtaa huu”
Bw. Magesa ameitaka kamati ya Ujenzi wa shule hiyo kufuatilia kwa ukaribu ujenzi wa shule hiyo ili kuepusha upotevu wa mifuko iliyotolewa na Mbunge KABATI.
“nikuhakikishie tu hakuna hata mfuko mmoja utakaopotea katika ujenzi wa madarasa ya shule hii, sisi na kamati ya ujenzi tutahakikishatunafikia malengo kwa kutumia saruji yote kama ulivyopanga”
No comments:
Post a Comment