Monday, February 24, 2020

DKT MABULA, BARABARA YA AIRPORT-KAYENZE-NYANGUGE KUANZA KUFANYIWA UPEMBUZI YAKINIFU MWAKA WA FEDHA UJAO.

Barabara ya kutoka uwanja wa ndege wa mkoa wa Mwanza kupitia Kayenze kuelekea Nyanguge yenye kilomita zaidi ya 46 inatarajiwa kuanza kufanyiwa upembuzi yakinifu kwa mwaka wa fedha ujao ili iweze  kujengwa kwa kiwango cha lami.

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya Kata ya Kayenze ambapo amesema kuwa Serikali inatarajia kuifanyia upembuzi yakinifu barabara hiyo ili ijengwe kwa kiwango cha Lami kurahisisha huduma ya mawasiliano baina ya wananchi wa maeneo hayo na kumaliza kero ya muda mrefu ya ubovu wa barabara iliyokuwa ikiwakabili wananchi hao

'.. Nashukuru Mungu ahadi niliyoitoa Kayenze ilikuwa ni kivuko na kwa bahat nzuri Mhe Rais Magufuli alisikia kilio chetu ametoa fedha na Kivuko kimekamilika, Jambo zuri zaidi na hii barabara yetu ya Kayenze wataanza kuifanyia upembuzi baadae wataijenga ..' Alisema

Aidha Dkt Mabula amewataka hofu wananchi wa Kayenze kuwa Kivuko cha Mv Ilemela kitaanza kufanya kazi hivi karibuni baada ya kukamilika kwa taratibu za kupanga nauli kesheria na kuzinduliwa rasmi na Serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Ilemela ambae pia ni mkazi wa kata ya Kayenze Ndugu Faida Bituro ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa utoaji wa fedha za mikopo ya vijana bila riba huku akimpongeza Mbunge Mabula kupitia taasisi iliyo chini ya ofisini yake ya The Angeline Foundation inayotekeleza  mradi wa ufatuaji  tofali, Kwa tofali walizotoa kwaajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Kayenze hivyo kutatua kero ya muda mrefu walikuwa wakiipata ya kufata huduma ya elimu kwa umbali mrefu.

Nae diwani wa kata ya Kayenze James Katoro amemshukuru mbunge huyo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea maendeleo wananchi wa kata yake huku akimuahidi ushirikiano kuhakikisha wananchi wake wanazidi kunufaika na uongozi wa awamu ya tano.

No comments:

Post a Comment