Saturday, February 22, 2020

CHAMA CHA MAPINDUZI CHAWAONYA WATUMISHI WA UMMA WAZEMBE PEMBA


CHAMA CHA MAPINDUZI CHAWAONYA WATUMISHI WA UMMA WAZEMBE NA WANAOCHELEWESHA MAENDELEO YA WATU – PEMBA
Akizungumza katika kikao cha ndani cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba Zanzibar, Ndugu Humphrey Polepole Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi amesema Chama Cha Mapinduzi kinawaonya Watumishi wa Umma wazembe, wanaochelewesha maendeleo ya Watu Pemba Zanzibar.

Akifafanua suala hilo Ndugu Polepole amesema pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Dk. Ali Mohammed Shein Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar bado wapo baadhi ya Watumishi wa Serikali wazembe wanaokwamisha kazi ya Serikali jambo ambalo linaweza kuteteresha heshima ya Chama katika Jamii.

Aidha Ndugu Polepole ametumia mkutano huo kusisitiza Wanachama na Viongozi wa Chama kuendeleza mshikamano wao, upendo, umoja na ikiwamo kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuyasemea mambo mazuri ambayo Serikali ya Mapinduzi inayafanya Pemba ili Chama kiendelee kupata ushindi wa kishindo na kusimamia utolewaji wa maendeleo.

Huu ni muendelezo wa ziara ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya Mwaka 2015 – 2020 Zanzibar.

No comments:

Post a Comment