Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda
akiongea na Wakazi wa Kilimanjaro wakati wa Uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha
wananchi kujiunga na mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya Mkoani Kilimanjaro,
ambapo aliwataka watanzania kutoweka rehani maisha yao katika suala la afya kwa
kukosa Bima ya Afya.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira akiongea na Wakazi wa Kilimanjaro
wakati wa Uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha wananchi kujiunga na mpango wa
Vifurushi vya Bima ya Afya Mkoani Kilimanjaro, ambapo aliwataka watanzania
kujiunga na Bima ya Afya kabla ya kuugua.
Wakazi
wa Mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia hafla ya Uzinduzi wa kampeni za kuhamasisha
wananchi kujiunga na mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya Mkoani humo.
Na
Mwandishi Wetu-KILIMANJARO
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF leo
umezindua kampeni ya kuhamaisha wananchi kujiunga na mpango wa vifurushi katika
Mkoa wa Kilimajaro.
Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Mama Anna Mghwira ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwataka watanzania
kujiunga na NHIF ili kuwa na uhakika wa matibabu badala ya kusubiri kuumwa
ndipo waanze kutafuta kadi ya bima ya afya.
“Wakati wa amani ambao ni wakati upo mzima
unatakiwa uwekeze na NHIF kwa kukata kadi ya Bima ya Afya na wakati wa vita
ambao ni wa maradhi NHIF ni wa uokoaji kwa kujitibia, jiungeni na NHIF ili tuwe
na uhakika wa matibabu"-Amesema RC Mghwira.
Aidha, RC Mghwira ameupongeza Uongozi wa
NHIF pamoja ma Bodi ya Mfuko huo kwa kuja na mpango huu wa vifurushi vya Bima
ya Afya ambao una lengo la kuwajumuisha watanzania wengi zaidi.
Akiongea katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Mama Anne Makinda amesema kuwa Mpango wa vifurushi
vya Bima ya Afya hauzuii taratibu nyingine za Serikali ikiwemo Sera ya Afya
inayotambua afya bure kwa watu wasio na uwezo ikiwemo Wazee.
Pia, Mama Makinda alisema kuwa Tanzania
sasa tunaingia katika makundi ya nchi ya uchumi wa kati hivyo mwananchi kuwa na
Bima ya Afya ni muhimu kwani nchi yoyote inayoendelea kuwa na Bima ya Afya ni
suala la msingi sana
Wakiongea kwa nyakati tofauti wanajumuiya
ya Machinga na waendesha bodaboda wameipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa
kuwajumuisha bodaboda na machinga katika mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya
ili na wao wanufaike na matibabu.
No comments:
Post a Comment