Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe akiwataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kujadili hoja zenye maslahi mapana kwa taifa alipokuwa akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi leo Jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi akiwasihi wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) kuhahisha wanawasilisha hoja zitakazo saidia kuboresha sekta za wizara na utendaji wakati wa ufunguzi wa baraza la wafanyakazi uliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw.Mfaume Said akiushukuru uongozi wa utawala wa wizara kwa kuboresha utendaji na kuwa karibu na wafanyakazi pamoja na kusikiliza kero zao katika ufunguzi wa baraza la wafanyakazi uliyofanyika leo jijini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe amewataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo kuwa wawazi katika mijadala ya mkutano huo kwa mambo ambayo hayaendi vizuri.
Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wenye lengo la kukumbushana, kuelimishana na kuweka mazingira bora ya utendaji kazi na kuweka umoja kati ya wafanyakazi na viongozi wa menejimenti.
“Katika Baraza hili ningependa muwe wawazi katika mijadala ya mambo yote yanayokwamisha utendaji wa majukumu ya wizara lengo ni kuhakikisha mazingira ya utendaji yanaboreshwa na kazi zinafanyika kwa manufaa ya taifa kwa wizara hii inamambo mengi yanagusa jamii moja kwa moja na hasa vijana tukiangalia sekta ya mfano Sanaa na Michezo,”alisema Dkt.Mwakyembe.
Naye Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Ally Possi aliwasitiza wafanyakazi wa waadilifu, kuepuka ubadhirifu na kufuata kanuni na taratibu za utumishi wa umma kwa kufanya hayo itasaidia kujenga mazingira yenye manufaa kwa wananchi na taifa kwa jumla.
“Mkutano wa baraza ni muhimu kwani unawaleta wafanyakazi na menejimenti pamoja hivyo basi kikao hichi kisitumimike kutafuta umaarufu badala yake utumike kujadili kwa kina namna ya kuboresha mazingira ya utendaji na mikakati ya itakayosaidia kuendeleza mbele sekta za wizara,’’alisema Dkt.Possi.
Pamoja na hayo Dkt.Possi liwasisitiza wajumbe hao wa baraza kutoa hoja zenye tija na maslahi kwa wizara huku akisema nimatarajio yake kuwa kikao hicho kitaibua fursa za namna ya kuboresha wizara na utendaji. Halikadhalika nae Mwenyekiti wa Tughe Tawi la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Mfaume Saidi aliushukuru uongozi wa wizara kwa kuboresha utendaji na
kuimarisha kuimarisha ushirikiano kwa wafanyakazi.
No comments:
Post a Comment