Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza
akizungumza na wadau wa tasnia ya filamu Mkoa wa Singida leo na
kuwasisitiza kurasimisha kazi zao pamoja na kujisajili,katika kikao cha kusikiliza kero za wadau hao na
kuwaeleza mikakati ya serikali katika
kuimarisha tasnia hiyo kilichoandaliwa
na Bodi ya Filamu Tanzania.
Naibu Waziri Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza
aliyeketi watatu kushoto akiwa
katika picha ya pamoja na wadau wa tasnia ya filamu Mkoani Singida leo mara
baaada ya kulamizika kikao cha kusikiliza kero za wadau hao na kueleza mipango
ya serikali katika kuimarisha sekta hiyo na kuthibibiti uharamia wa kazi za
filamu na kuhakikisha msanii ananufaika na kazi yake,wa pili kulia Kaimu ni
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo pamoja na Katibu
Tawala Wilaya ya Singida Wilson Shimo.
Naibu
Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (aliyeketi wapili kushoto) akimsikiliza Msanii wa Filamu Mkoa wa Singida
Bi.Maria Luya akimweleza stori ya kuhusu
filamu yake iitwayo furaha kabla ya kumkadhi leo katika kikao chake na wadau
hao wa filamu kilichofanyika Mkoani Singida,wa kwanza kulia ni Katibu Tawala Wilaya
ya Singida Wilson Shimo na wa pili kulia ni Kaimu ni Katibu Mtendaji Bodi ya
Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo.
Na Anitha Jonas – WHUSM, Singida
Naibu Waziri Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana
Shonza amewasisitiza wanatasnia ya filamu kuhakikisha wanarasimisha kazi zao na
kujisajili.
Mheshimiwa Shonza ametoa agizo hiyo leo
Mkoani Singida alipokuwa akifanya kikao na wadau wa
tasnia ya filamu wa mkoa huo kwa lengo la kutaka kusikiliza kero zao na
kuwaeleza wadau hao mikakati ya serikali katika kuboresha tasnia hiyo,kuthibiti
uharamia ili kuhakikisha wanafaidika na
kazi zao.
Akiendelea kuzungumza katika kikao
hicho Naibu Waziri huyo aliwasisitiza wanatasnia hao wa filamu kuzingatia suala
la uandaaji wa muswada wa filamu na kupeleka miswada hiyo kwa maafisa utamaduni kwa ajili ya ukaguzi na kupata ushauri wa
filamu watakayoandaa sababu hiyo ni moja
ya njia itakayosaidia kuandaa kazi zenye ubora.
“Kwanza ningependa niwashauri muache
kusambaza au kuuza kazi zenu kwa njia ya ‘flash’ katika vibanda vya kuuza
filamu sababu hii bado ni njia inayowakandamiza na hauwezi kupata faida ya kazi
yako, sasa hivi kazi hizo za filamu zinasambazwa kwa mfumo wa kidigitali mfano
kwenye Swahilifilx na Netflix,kikubwa ni kazi yako iwe yenye ubora na
iliyozingatia utaratibu wa kitaalamu katika kuandaa filamu ikiwemo
wachezaji kuvaa uhusika na kucheza
katika maeneo yenye uhalisia wa filamu hiyo,”alisema Mhe.Shonza.
Naye Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya
Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo bodi imekuwa ikitoa mafunzo kwa wadau wa tasnia
hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandaa kazi bora zitakazo kuwa na
ushindani kwa ndani na nje ya nchi na kwa hivi karibuni wanatarajia kufanya
mafunzo hayo mkoani Dodoma na kwa wadau wa Singida ambao hawajawahi kupata
mafunzo hayo wanakaribishwa kushiriki.
“Bodi ya filamu katika kuimarisha
masoko ya usambazaji wa filamu ndani na nje ya nchi imempata mdau kutoka Nigeria mwenye Kampuni iitwayo ENVIVO ambaye yupo tayari
kununua jumla kazi mia moja mpaka
ifikapo mwezi Juni mwaka huu,zenye hadithi mbalimbali za kitanzania ambapo zitatafsiriwa
kwa lugha kwa lugha ya Yoruba,Pijini na
Igbo kusambazwa,kikubwa katika kazi hizo ni ziwe zimebeba hadithi za kitanzania
na zenye ubora na pia ziwezinaendana na
muswada,”alisema Dkt.Kilonzo.
Pamoja na hayo Dkt.Kilonzo aliwasihii
wadau hao kuwa mfumo wa usambazajiwa kwa kazi za filamu kwa sasa umebadilika na
filamu kwa sasa mara baada ya kukamilika inafanyiwa uzinduzi katika majumba ya
sinema na huko itaonyeshwa kwa kipindi fulani na baadae inapelekwa katika
mifumo mingine ya kidigitali na hatua ya kuiweka katika CD na Youtube
niyamwisho hii ni katika kulinda kazi hizo na uharamia pia kuhakikisha msanii
anapata faida ya kazi yake.
Kwa upande wa Afisa Utamaduni Mkoa
Bw.Hendry Kapera alisema wasanii wengi wa filamu katika mkoa huo hawataki
kujisajili wala kurasimisha kazi zao hii ni changamoto kubwa na wamekuwa wakijiweka
mbali na maafisa utamaduni wa wakihofia kuulizwa kuhusu usajili na hii
imechangia wao kuandaa kazi zisizo na ubora sababu hawapendi kushirikiana na
maafisa hao.
Halikadhilika nae mmoja ya wasanii hao
wa filamu kutoka Wilaya ya Ikungi
Bw.Salumu Ntandu aliomba bodi ya filamu kuwapatia mafunzo wadau hao wa
mkoa huo na pia aliwasihii wasanii wenzake kuwa na umoja na kuacha migogoro
kwani umoja wao ndiyo utakaoweza kutangaza kazi zao na kutangaza mkoa wao pale
watakapo andaa kazi nzuri zenye ubora na kushirikishana katika kuitangaza na kuizindua.
No comments:
Post a Comment