Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifungua mkutano wa wa wadau
wa kujadili mpango wa kuhamasisha matumizi ya Gesi Asilia nchini,
uliofanyika Jijini DSM.
Kamishna wa Petroli na Gesi, Adam Zuberi akizungumza na waandishi wa
wabari wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mpango wa kuhamasisha
matumizi ya Gesi Asilia nchini, uliofanyika Jijini DSM
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akipokea jarida maalumu
lenye taarifa mbalimbali zinazohusu Shirika la Maendeleo la Japani, (JICA)
kutoka kwa mwakilishi Shirika hilo, Naofumi Yamamura
Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu( kulia) na Kamishna wa Petroli na
Gesi wa Wizara ya Nishati, Adam Zuberi wakifuatilia mada zilizokuwa
zikitolewa wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mpango wa
kuhamasisha matumizi ya Gesi Asilia nchini, uliofanyika Jijini DSM
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, amesema tayari Serikali
imekamilisha mpango wa awali wa kusambaza gesi kwenye Mikoa mitano
ili kuhakikisha kuwa Tanzania inatumia rasilimali hiyo inayochimbwa nchini
katika kuimarisha uchumi wa viwanda.
Mgalu alisema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa kujadili
mpango wa kuhamasisha matumizi ya Gesi Asilia nchini, uliofanyika Jijini
DSM, Januari 17,2020.
Mgalu alisisitiza kuwa mpango huo ni matokeo ya utafiti wa miaka mitatu,
uliofanywa na Serikali kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la
Japan (JICA).
Aliitaja Mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro na
Morogoro.
Aidha alieleza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha mikoa yote Tanzania
inapata nishati hiyo kwa matumizi mbalimbali.
"Tanzania tumegundua gesi asili yenye ujazo wa futi trilioni 57 hii sasa
tunaitengenezea mkakati wa matumizi yake,
Kwa mijiibu wa takwimu zinaeleza kuwa mpaka sasa gesi asilia
inayochiimbwa chini inazalisha Megawati 892.72 sawa na 57 % ya
Megawati zote zinazozalishwa.
Aliweka wazi kuwa Gesi Asilia inatumika pia kwenye magari, tumeanza
hapa Dar es Salaam ambapo magari takribani 200 yanatumia gesi na
miundombinu ya kusambaza gesi hiyo inaendelea kuboreshwa ili
kuwasogezea huduma watumiaji, na hii ndio maana hasa ya utafiti huu.
"Gesi asilia inatusaidia pia kutunza mazingira hasa kwenye kupikia
ambapo mpaka sasa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),
limesambaza miundombinu ya gesi ya kupikia majumbani katika Mikoa ya
Lindi, Mtwara, Dar es Salaam na Pwani," alisisitiza Mgalu.
Kuhusu matumizi ya gesi viwandani Mgalu alisema viwanda zaidi ya 50
vimeunganishwa na gesi asilia.
"Huu ni mradi mkubwa Sana utakuwa wa muda mrefu pia hadi kufikia
mwaka 2046 tangu kuanza kwa mradi huu mwaka 2017.
Kwa upande wake Kamishna wa Petroli na Gesi wa Wizara ya Nishati ,
Adam Zuberi alisema Tanzania ipo kwenye wakati sahihi hivyo jitihada za
makusudi zinafanyika kufikisha gesi asilia kwenye mikoa yote Tanzania.
"Tupo katika Muda muafaka wa utafiti huu unaolenga kuhakikisha kwamba
Mikoa yote nchini inapata na kutumia gesi asilia kwa njia bora na sahihi,"
alisema Zuberi.
Mshauri wa Taasisi ya Nishati na Uchumi kutoka Japan, Kensuke
Kanekinyo alisema awamu ya kwanza ya mradi huo imetumia Dola Milioni
mbili za Marekani kwa miaka mitatu.
Alisema gharama za mradi wote ni Dola milioni 250 zitakazotumika
kupeleka gesi mikoa yote ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment