Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akioneshwa jinsi umeme
unavyosaidia kurahisisha kazi ya kuchenjua dhahabu kwa kutumia
teknolojia ya kisasa katika mgodi wa Mwabomba wilayani Kahama mkoani
Shinyanga.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (kulia) akipitishwa na mmiliki
mgodi na mtambo wa uchenjuaji dhahabu wa Mwabomba (kushoto) katika
sehemu ya mtambo huo unatumia umeme kuendesha shughuli za
uchenjuji dhahabu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambayo ni rafiki kwa
binadamu na mazingira.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (katikati) akikata utepe na
kuwasha umeme katika mgodi na mtambo ya kuchenjua madini ya
dhahabu wa Mwabomba wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Imeelezwa kuwa dhamira ya Serikali katika kuwainua wachimbaji wadogo
kwa kuwaunganishia huduma ya umeme katika migodi na mitambo ya
kuchenjulia dhahabu ili kuwapunguzia gharama za uendeshaji na kupata
faida kubwa zaidi.
Dhamira hiyo ilidhihirishwa wazi na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani, Januari 24, 2020, wakati akiwasha umeme katika mgodi na
mtambo wa kuchenjua dhahabu wa 136 kuwashiwa umeme nchi nzima
uliopo katika Kijiji cha Mwabomba wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Dkt. Kalemani alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano kupitia sera ya
uchumi wa viwanda imedhamiria kuwainua na kuwathamini zaidi
wachimbaji wadogo kwa kuhakikisha inawaunganishia umeme wa bei
nafuu wale wote wenye migodi na mitambo ya kuchenjua dhahabu, ili
umeme huo uwarahisishie shughuli za uendeshaji na kuinua vipato vyao.
Alisema umeme katika sehemu za migodi utampunguzia mchimbaji mdogo
gharama za uendeshaji na kupata faida ambayo pia atalipa kodi na tozo
mbalimbali za serikali bila vikwazo na kuiongezea serikali mapato.
;Tutahakisha migodi na mitambo yote ya kichenjua dhahabu au madini ya
aina yeyote ile hapa nchini inaunganishiwa umeme, hii itasaidia pia kuwa
wachimbaji wa kisasa zaidi kwa kutumia teknolojia bora ambazo
hazitaruhusu hata chembe ya madini yao kupotea, na teknolojia hizo ni
rafiki kwa binadamu na mazingira kwa jumla, bila umeme technolojia
nyingine hawataweza kuzitumia", alisema Dkt. Kalemani.
Akizungumzia usambazaji wa umeme vijijini, Waziri aliliagiza Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) kuunganisha kata zote 20 ambazo
hazijaunganishwa na umeme hadi kufikia mwezi Aprili mwaka huu katika
Wilaya ya Kahama.
Alieleza kuwa wananchi hawataki kusikia habari ya aina yeyote juu ya
umeme, zaidi ya kuona unawaka ndani ya majumba yao na hakuna sababu
ya msingi ya kuwafanya wananchi hao wakose umeme kwa kuwa tayari
fedha zipo na vifaa vyote vinapatikana hapa nchini na watalaamu wa kazi
hiyo wapo.
Mapema akiwa katika ziara hiyo wilayani Nyang'hwale, mkoani Geita, Dkt.
Kalemani, aliiagiza (TANESCO) kukamilisha ufungaji wa mashineumba
(Transfoma) na kuwasha umeme katika mgodi wa Nyamigongo ambao
hutumia zaidi ya shilingi milioni 120 kwa mwezi ikiwa ni gharama za
kununua Mafuta ya kuendesha shughuli za Uzalishaji tofauti na umeme
angetumia takribani milioni 80.
Aliwaeleza TANESCO kuwa, mashineumba watakayofunga si kwamba
itamnufaisha mwekezaji huyo pekee, bali zaidi ya vijiji 20 vinavyomzunguka
vitatumia mashineumba hiyo kuwasambazia umeme. Aidha, shirika hilo
litapata faida kubwa itakayowawezesha kuendelea kusambaza umeme na
kuboresha miundombinu iliyochakaa ama kuharibika.
Kwa upande wao wamiliki wa migodi hiyo, wameishukuru serikali kwa
kuwathamini wachimbaji wadogo ambao walikuwa kama wametelekezwa
katika kutatuliwa matatizo na changamoto mbalimbali zinazowakabili
ikiwamo kuboreshwa kwa shughuli zao za uchimbani kwa manufaa zaidi.
Vilevile, akiwa Wilayani, Nyang'hwale Waziri huo wa Nishati, aliwasha
umeme katika shule ya msingi iliyoanzishwa mwaka 1958 takribani miaka
62.
Aidha, alitembelea eneo linalojengwa Makao Makuu ya Wilaya ya
Nyang’hwale, Hospitali na majengo mengine ya serikali na kuagiza
TANESCO kufunga mashineumba yenye uwezo mkubwa katika eneo hilo
ili iharakishe shunguli za kiutendaji.
Pia, alimuagiza mkandarasi anayetekeleza mradi wa usambazaji umeme
vijijini katika wilaya hiyo, kuongeza kasi ya kuunganishia umeme mara tuu
baada wateja kuliolipia na kuongeza kasi ya usambazaji umeme katika
vijijini wanavyotekeleza mradi huo na kuwasha vijiji vitatu kila wiki.
Vilevile, alimtaka kuondoa nguzo zilizorundikwa sehemu moja kwa muda
mrefu na kuzisambaza katika maeneo mbalimbali zinapohitajika na endapo
ni mbovu basi azirudishe kwa walikozinunua ili wapatiwe nguzo zingine
kulinagana na makubaliano yanavyoelekeza.
Kwa upande wake, mkuu wa wilaya hiyo, Hamim Gwiyama alimuhakikishia
Waziri huo kuwa kabla ya majengo hayo kukamilika watalipia gharama za
uunganishaji umeme katika majengo ili umeme huo pia usaidie shughuli za
umaliziaji ujenzi wa majengo hayo.
Vilevile, wataendelea kulipia Taasisi za Umma kama shule, vituo vya Afya
na Taasisi za Dini zilizopo katika maeneo yao ili ziunganishiwe umeme.
No comments:
Post a Comment