Sunday, January 5, 2020

ENG MTIGUMWE, AKERWA NA UZEMBE ULIOPELEKEA MGOGORO WA WAKULIMA MANG’OLA



Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe amelazimika kuingilia kati mgogoro wa wakulima Kata ya Mang’ola wilayani Karatu mkoani Arusha uliosababishwa na halmashauri na wakulima kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati kitendo ambacho kingepelekea kukauka kwa skimu za maji, wakulima kushindwa kufanya uzalishaji na kuikosesha serikali mapato kwani wakulima wa maeneo hayo hutegemea umwagiliaji katika kilimo cha vitunguu na mazao mengine.

Akizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe Theresia Mahongo,watumishi ya halmashauri hiyo na baadae na wakulima wa Kata ya Mang’ola na Kata ya Baray amesemakuwa yeye kama mwakilishi na mtendaji mkuu wa Wizara ya Kilimo,wizara inayosimamia kilimo na umwagiliaji amelazimika kufika eno hilo kuona ninamna gani changamoto za vita ya kugombania maji ya chanzo cha Mto Mang’ola katika umwagiliaji zinatatuliwa kwa haraka.

Ameongeza kuwa skimu hizo za umwagiliaji ni muhimu sana kwa wilaya ya Karatu katika Kilimo na kuongeza mapato kwenye halmashauri hiyo endapo migigoro iliyopo itatatuliwa kwa wakati na kuhakikisha wakulima wanasaidiwa kutatua changamoto zinazo wakabili katika uzalishaji na masokona.

Mtigumwe ameongeza Mang’ola ni katika maeneo ambayo wakulima wamehamasika kulima kwa wingi kulinganisha na maeneo ambayo skimu  zimepelekwa lakini watu hawakuhamasika kulima lakina katika skimu hizi za Mang’ola watu wamehamasika kufanya uzalishaji  kwa kutumia umwagiliaji na ndo maana nimehamasika kutembelea eneo hili ili kutatua migogoro.

Amesemakuwa viongozi mbalimbali wameshafika lakini sisi kama wizara tumeamua tuje tuone ni namna gan tunaeza shirikiana na halmashauri,wakulima,wizara na tume ya umwagiliaji tutakaa kwa pamoja ili tuone namna gan tunaeza kuondoa vikwazo ambavyo vinasababisha tunashindwa kufikia malengo katika uzalishaji sisi kama wizara,halmashauri na wakulima kwa ujumla.

Amesema kuwa jukumu la kuhakikisha tunazalisha sana kwenye eneo hili la ekta elfu tano mpaka elf sita la wilaya ya karatu ni jukumu la serikali,wizara ya kilimo,wilaya,mkoa,tume ya umwagiliaji,wananchi na wadau wote wa kilimo

Katika changamoto zote zilizopo kila mtu anahusika kuzitatua changamoto hizo ukkwani kunasehemu ambazo halmashauri ilitakiwa ifanye hawakufanya sana na sehemu ya wananchi kufanya majukumu yao hawakufanya aidha kwa kukosa maelekezo wangeweza kufanya kitu Fulani hawakufanya hivyo kupelekea migogoro iliyogarimu serikali na wakulima.

“ni lazima tuhakikishe eneo hili linazalisha zaidi na kuhakikisha changamoto hizi tunazitatua, kunaambazo tunaweza kuzitatua leo hii lakini kunazingine lazima tuendenazo na tukirudi hapa mwezi wa kumi na mbili mwaka huu kila mmoja wenu awe amefanya kwa nafasi yake na kukamilisha majukumu yake ipasavyo”amesema mhandisi Mtigumwe.

Mtigumwe akizungumzia upungufu wa maji katika skimu amesema changamoto hiyo imepelekea kuleta  mgogoro kwa wakazi wa maeneo hayo kwa kugombea zamu za umwagiliaji hivyo ni vyema kubuni mbinu mpya za kuongeza vyanzo vya maji kama kuchimba visima vingi na kuimarisha vyanzo vya maji na kuchimba bwawa kwaajili ya kuhifadhi maji.

Ambapo katika hatua hiyo ameiagiza tume ya umwagiliaji kufanya tathimini katika skimu hizo za umwagiliaji na kuona ni namnagani upatikanaji wa maji unaweza kuongezeka kupitia vyanzo vya maji vilivyopo kabla ya kuanza utekelezaji wa kuchimba visima ambavyo halmashauri,tume ya umwagiliaji na Wizara ya Kilimo zitahusika.

Aidha ameitaka halmashauri,wakulima na tume ya umwagiliaji kuhakikisha wanafanya majukumu yao ipasavyo ili kuepukana na migogoro kuendelea tena baada ya ufumbuzi alio utoa.

Kata hizo mbili zinaundwa na vijiji sita ambavyo ni Mang’ola Barazani, Malekchand, Laghangareni vilivyopo Kata ya Mang’ola na vijijini vya Jobaj, Dumbechand na Qangdenda vilivyopo kata ya Baray.

Wananchi wa vijijini hivyo wanaodaiwa kufikia 30,000 wameingia katika mgogoro wa kugombania maji ya Mto Mang’ola yanayotumika kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji cha vitunguu pamoja na mazao mengine.

No comments:

Post a Comment