Mkurugenzi
Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe
akisisitiza umuhimu wa Mipango ya kujiandaa na kukabiliana na maafa ya Mikoa
linakopita Bomba la Mafuta, kuzingatia athari zinazoweza kujitokeza na kuathiri
Mradi huo, wakati alipotembelea eneo la kwenye peninsula ya Chongoleani
karibu na bandari ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa .
Mkurugenzi
Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe
akisisitiza umuhimu wa Mipango ya kujiandaa na kukabiliana na maafa ya Mikoa
linakopita Bomba la Mafuta, kuzingatia athari zinazoweza kujitokeza na kuathiri
Mradi huo, wakati alipotembelea eneo la kwenye peninsula ya Chongoleani
karibu na bandari ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa.
Ofisi ya
Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, imezishauri Kamati za Usimamizi wa
Maafa katika mikoa 8 na vijiji 184 vinavyopatikana
katika wilaya 24 zilizopo katika mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora,
Singida, Dodoma, Manyara na Tanga, ambapo Mradi wa Bomba la Mafuta utatekelezwa
kuuweka Mradi huo katika Mipango yao ya kujiandaa na kukabiliana na Maafa ili
kuhakikisha mradi huo hauthiriwi na majanga yanayoweza kutokea.
Kwa mujibu
wa sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha majukumu
ya kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa, ambapo
kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutoa taarifa za tahadhari ndani
ya eneo husika, Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa maafa na
operesheni za dharura ndani ya Kijiji wilaya au mkoa, pamoja na kutafuta
rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika ngazi husika.
Akiongea
mara baada ya kutembelea eneo la kwenye peninsula ya Chongoleani karibu na
bandari ya Tanga ambapo utekelezaji wa Mradi huo utatekelezwa, Mkurugenzi Idara
ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amefafanua
kuwa Kamati za maafa zinalo jukumu la kuchukua tahadhari ya namna ya
kuhakikisha majanga yanayoweza kuuathiri mradi huo yanakuwa katika mipango yao
ya menejimenti ya maafa ili faida zitakazotokana na utelelezaji wa mradi huo
zinakuwa endelevu.
Kwa upande
wake, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Noel Kazimoto ameeleza
kuwa utekelezaji wa mradi huo utafungua fursa za kiuchumi kwa watanzania hivyo
ni dhahiri kuwa eneo la Chongoleani litakuwa na mwingiliano mkubwa wa watu na
shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii zitakuwa zikiendeshwa, kwa kuwa wananchi
ni wadau wa menejimeti ya maafa kupitia kamati za menejimenti za
maafa kuanzia ngazi ya vijiji, wataendelea kuelimishwa juu ya
majanga yanayoweza kuuathiri mradi huo ili waweze kuhakikisha mradi
unakuwa endelevu.
Kwa mujibu
wa Tovuti rasmi ya Kampuni inayojenga mradi huo, East African Crude Oil
Pipeline www.eacop.com.
Kampuni hiyo inabainisha kuwa wanao mpango unaohakikisha utelezaji wa mradi huo
unazingatia majanga na maafa wakati wa kupanga, kujenga na kuendesha Bomba,
ambapo Mpango huo unahakikisha kwamba, katika tukio la dharura linaloweza
kutokea, hatua za haraka, zinachukuliwa.
Mradi wa
Bomba la Mafuta Ghafi unatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikisha
kampuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikali
za Tanzania na Uganda. Mafuta ghafi yatasafirshwa kutoka Kabaale katika
Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. Mradi
wa Bomba hilo una umbali wa kilometa 1,445 ambapo kilometa 298 zitakuwa nchini
Uganda, na kilometa 1,147 zitakuwa nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment