Na Mathias
Canal, NFRA
Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya chakula uliingia
mkataba wa kuuza tani 17,000 za mahindi na Serikali ya Zimbabwe tarehe 02
Septemba, 2019 Ilikubaliwa kuwa tani zote zitatoka kwenye kanda ya makambako kadhalika
kanda hiyo ilipewa jukumu la kusimamia upakiaji wa mahindi kwenye mabehewa ya
TAZARA tayari kwa kusafirisha kwenda Bulawayo Harare Zimbabwe.
Kanda ya
makambako inavyo vituo vikuu viwili vya kuhifadhia ambavyo ni Makambako na Mbozi katika utekelezaji wa mkataba huo ilikubaliwa tani 7,000 zichukuliwe kutoka kituo cha
Makambako, na tani 10,000 kutoka kituo cha Mbozi.
Kazi rasmi ya kupakia kwenye behewa na
kusafirisha mahindi kwenda Zimbabwe ilianza tarehe 17 Septemba, 2019
na ilianza kwenye kituo cha Makambako kwa kuwa TAZARA walikuwa wameandaa
mabehewa tayari kwenye kituo hicho. Upakiaji kwenye kituo cha Mbozi ulianza
tarehe 20 Septemba, 2019
Utekelezaji wa tani 7,000 kituo cha makambako
ulimalizika tarehe 25 oktoba, 2019
lakini kituo cha Mbozi ambacho
kilipangiwa kutoa tani 10,000 kazi ilimalizika tarehe 26 Novemba, 2019.
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) umefanikiwa
kutekeleza mkataba kwa asilimia 100, hadi kufikia tarehe 26.11.2019 ambapo kiasi
cha tani 17,000 zilikuwa zimeshapakiwa nakukabidhiwa kwa wasimamizi wa
mzigo tayari kwenda Bulawayo Harare –Zimbabwe.
Muda wa kutekeleza mkataba ulikuwa ni siku 120 kuanzia
tarehe 02.09.2019 hata hivyo Wakala umetekeleza kwa siku 86.
NFRA ilikuwa na uwezo wa kutekeleza mkataba huo ndani
ya miezi miwili tu, kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza mkataba
huo ulifikia siku 86.
Changamoto zilizojitokeza ni pamoja na Ucheleweshaji
wa mabehewa, Uchache wa maturubai ya kufunikia mabehewa, na Hali ya hewa
kubadilika mara kwa mara kutokana na msimu wa mvua.
MWISHO
No comments:
Post a Comment