Katibu Mkuu wa Uvuvi Dk.Rashid
Tamatamah, kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.akizungumza wakati alipokuwa
akifungua warsha ya kuimarisha kilimo na biashara ya mwani kwa wadau
mbalimbali ikiwemo wabunge na makampuni yanayojishughulisha na zao hilo,
iliyofanyika jijini Dodoma.
Meneja wa kampuni ya Mwani
Mariculture Ltd, Hamil Said Soud,akitoa taarifa wakati wa ufunguzi wa
warsha ya kuimarisha kilimo na biashara ya mwani kwa wadau mbalimbali
ikiwemo wabunge na makampuni yanayojishughulisha na zao hilo,
iliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu washiriki wakifatilia
warsha ya kuimarisha kilimo na biashara ya mwani kwa wadau mbalimbali
ikiwemo wabunge na makampuni yanayojishughulisha na zao hilo,
iliyofanyika jijini Dodoma.
……………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imesema
ipo kwenye mchakato wa kuanzisha sheria mpya ya ukuzaji viumbe
maji(Aquaculture Act) ambapo pamoja na mambo mengine kutakuwa na
vipengele vinavyoratibu shughuli za uzalishaji na biashara ya zao la
mwani.
Aidha, imewataka wadau wa zao la
mwani kuhakikisha biashara ya zao hilo inafanyika kwa amani na uaminifu
kwa kufuata sheria zilizopo ili iwe na tija kwa kila mmoja.
Hayo yameelezwa leo na Katibu Mkuu
wa Uvuvi Dk.Rashid Tamatamah alipokuwa akifungua warsha ya kuimarisha
kilimo na biashara ya mwani kwa wadau mbalimbali ikiwemo wabunge na
makampuni yanayojishughulisha na zao hilo, iliyofanyika jijini Dodoma.
Amesema awali mafanikio makubwa ya
zao hilo yalipatikana kwa haraka na kuipaisha Tanzania hususan Zanzibar
kama mzalishaji mkuu wa zao hilo duniani ikifuatiwa na ufilipino.
“Mpaka kufikia mwaka 2006
walikuwepo wakulipa zaidi ya 300 Tanzania bara na zaidi ya 20,000 kwa
Zanzibar, wengi wao wakiwa ni wanawake.Lakini kutokana na changamoto
mbalimbali miaka ya hivi karibuni uzalishaji umeshuka na Tanzania sasa
ni ya tatu baada ya Ufilipino na Indonesia,”amesema.
Ametolea mfano kwa upande wa
Tanzania bara uzalishaji ulishuka hadi tani 918 katika mwaka 2018/19
ikilinganishwa na tani 1,329.5 mwaka 2017/18 na tani 1,197.5 mwaka
2016/17 au tani 1,500 zilizovunwa mwaka 2004/5.
“Upungufu katika uzalishaji
uliojitokeza umesababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo
mabadiliko ya hali ya hewa, ukosefu wa mitaji na wawekezaji makini,
ununuzi wa mwani usiofuata taratibu na kutokuwa na soko la
ndani,”amesema.
Kufuatia hali hiyo, Katibu huyo
amesema serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufanya tafiti
zinazolenga kupunguza changamoto na kuwajengea uwezo wakulima ikiwa ni
pamoja na fursa za mikopo na kuongeza kasi katika kutafuta masoko mapya.
Pia amesema kuanzishwa kwa Dawati
la Sekta binafsi Wizarani mwaka 2018 kumesaidia kwa kiasi kikubwa
kuziunganisha taasisi za fedha na wakulima na wafugaji kwenye tasnia ya
ukuzaji viumbe maji kwa ajili ya upatikanaji wa mikopo na mitaji.
“Lakini pia tafiti zinazofanywa na
taasisi yetu ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania(TAFIRI) kwa kushirikiana na
Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam zimesaidia
wakulima jinsi ya kukabiliana na kupunguza athari ya mabadiliko ya tabia
nchi na kusaidia kuongeza uzalishaji wa zao la mwani,”amesema.
Kwa upande wake, Meneja wa
kampuni ya Mwani Mariculture Ltd, Hamil Said Soud, amesema masuala ya
masoko ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili.
“Wawekezaji wawekewe mazingira
wezeshi kwa kuwa uzalishaji unashuka, tunatakiwa kujiuliza ni kitu gani
kinachoshusha uzalishaji? Tunatakiwa kuhakikisha wawekezaji wanapokuja
wawekewe mazingira wezeshi kwa kuwa kuna nchi kama Kenya zimeanza
uzalishaji baada ya sisi lakini zinakuja kwa kasi sisi uzalishaji
unashuka,”amesema.
Naye, Mbunge wa Mchinga(CUF),
Hamidu Bobali amesema changamoto kubwa wakulima wanakabiliwa na shida ya
kamba ambapo kamba moja inauzwa Sh.10,000.
“Wawekezaji wanatakiwa kuhakikisha
bei ya kamba inashuka inakuwa ya wastani na wahakikishe wakulima
wanakuwa na kamba, kilimo hichi kinafanywa na watu wenye vipato vya
chini hasa kina mama, pia wawekezaji wasaidie kuwepo na maeneo ya
kuanikia mwani,”amesema.
No comments:
Post a Comment